logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Sidhani kama nitakuwa mjamzito tena, mwakani nitafunga mirija yangu ya uzazi” – Murugi Munyi

Munyi alisherehekea kufikisha umri wa miaka 34 mwezi Mschi tarehe 2 mwaka huu.

image
na Davis Ojiambo

Burudani07 August 2024 - 06:07

Muhtasari


  • • Alibainisha haya baada ya mashabiki wake kuzua dhana za tangazo la mimba baada yake kuenda Instagram Live.
MURUGI MUNYI

Mjasiriamali Murugi Munyi ametangaza nia yake ya kuziba mirija yake ya uzazi mwaka ujao.

Kupitia Istagram Live, Munyi alitangaza kwamba hana mimba na wala hatarajii kuwa mjamzito tena katika maisha yake, akiweka wazi kwamba katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mwaka ujao, jambo moja ambalo atajifanyia ni kufunga mirija yake ya uzazi.

Alibainisha haya baada ya mashabiki wake kuzua dhana za tangazo la mimba baada yake kuenda Instagram Live.

Alisema kwamba mashabiki wengi wamekuwa na dhana katika fikira zao kwamba mtu akifanya Instagram Live kutoa tangazo basi moja kwa moja wanakisia kwamba ni taarifa kama si za ujauzito basi ni za kuachana na mpenzi wake.

“Sababu kuu ya kufanya hii Instagram Live ni kuwapa taarifa kuhusu mabadiliko makubwa ambayo ninataka kufanya katika maisha yangu. Hapana siko mjamzito, sina mtoto katika tumbo langu, mume wangu na mimi hatuna mpango wa kutalikiana, na hakuna kitu kimetokea kwa watoto wangu,” alisema.

“Napenda jinsi mtu anavyosema ako Instagram Live watu wanaanza kuzua moja kwa moja kwamba ni mjamzito. Nyinyi watu kwani hamkuona tumbo langu lilivyo laini katika picha zangu nikiwa kwenye gym?”

“Kusema kweli siwezi kuwa mjamzito tena watu wangu. Sina mimba, sipangi kuwa na mimba na hakuna uwezekano kuwa nitawahi kuwa mjamzito tena katika maisha yangu. Na nimesema kwa siku yangu ya kuzaliwa mwaka ujao Machi napanga kufunga mirija yangu ya uzazi,” alimaliza.

Mjasiriamali huyo anajulikana sana kwa kuwa celeb wa kwanza Kenya kuweka wazi kuhusu mchakato wake wa kufanya upasuaji wa liposuction kupunguza mafuta kwenye mwili wake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved