logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jabidii: Nilipata mirabaha ya 2k kutoka kwa Odi Dance licha ya kuwa 'viral hit'

Kwanza ilinipiga shock ikanihit manze muziki is a scam.

image
na Davis Ojiambo

Burudani08 August 2024 - 05:35

Muhtasari


  • • Kutokana na ukweli huo machoni pake, Jabidii alisema alihisi kabisa muziki ni utapeli na hata akawaza kuachana nao.
Jabidii

Msanii wa injili ya kisasi kipya humu nchini, Jabidii amefichua jinsi alihisi kukata tamaa ya kufanya muziki baada ya Mapato duni ya mirabaha.

Akizungumza na Dr Ofweneke kwenye runinga ya TV47, Jabidii alifichua kwamba alipata mirabaha ya shilingi eldu 2 pekee kutoka kwa ngoma yake ya kwanza ku'hit, Odi Dance.

Msanii huyo alisema alijihisi vibaya kupokea kiasi hicho kidogo kutoka kwa mamlaka inayosimamia hakimiliki za kazi za Sanaa, kwani kupindi hicho wimbo huo ulikuwa maarufu kila mahali na zaidi ya yote kushinda tuzo ainati.

"Nilipigwa 2k manze na CMOs, kwanza nilishtuka manze juu kuangalia hii song yangu ndio imepiga number one kila mahali, imeshinda Groove Awards, halafu ukiangalia wame wamekuwa ranked kwamba huyu ndio amekula the highest, ilinipiga shock," Jabidii alisema.

Kutokana na ukweli huo machoni pake, Jabidii alisema alihisi kabisa muziki ni utapeli na hata akawaza kuachana nao.

"Kwanza ilinipiga shock ikanihit manze muziki is a scam. Lakini with time timetoa hizo ngoma zingine, Vimbada, Makofi....so hatuwezi ngoja kuna ngoma ingine itakuja kubadilisha life. So all this time nimelearn kusurvive bila sijui nangoja royalty kutoka wapi na wapi," aliongeza.

Kwa sasa msanii huyo wa hit song ya Makofi anazidi kitamba ya kibao cha 'Miel Matin' ambacho ameshirikiana na mamake, Ayun Nyapolo na kuwavutia wengi haswa kwenye jukwaa la TikTok. 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved