• Sosuun alionyesha kujuta zaidi akisema kuwa endapo njia zilikuwa zinaambia watu pa kwenda, yeye angechukua njia tofauti na kukwepa ile iliyomuelekeza katika huba la Kenrazy.
Rapa wa Kike humu nchini Sosuun kwa mara nyingine amerusha dongo kwa aliyekuwa moenzi wake, msanii Kenrazy.
Kupitia Instagram yake, Sosuun alichapisha picha ya ukaribu ya uso wake na kudai kwamba anajuta kuolewa na Kenrazy ikizingatiwa urembo mkubwa alionao.
"Na hii sura yangu nzuri, majuto yangu makubwa ni kuolewa na Kenrazy na kukubali kuolewa katika familia ambayo haikuonyesha hata chembe ya mapenzi kwa binadamu ambaye alipenda kila mmoja wao na hata kuwazalia mabinti warembo," Sosuun aliandika.
Mama huyo wa mabinti 2 alizidi kuzua wasiwasi akisema kwamba endapo chochote kibaya kutamsibu, kila mtu anajua mhusika na mahali pa Kuanzia kumtafuta.
Sosuun alionyesha kujuta zaidi akisema kuwa endapo njia zilikuwa zinaambia watu pa kwenda, yeye angechukua njia tofauti na kukwepa ile iliyomuelekeza katika huba la Kenrazy.
"Kama kitu kibaya kitawahi nitokea, nyinyi wote mnajua pa kutafuta majibu. Mungu wangu, ikiwa barabara zingekuwa zinaambia watembeaji mahali pa kutoenda, ningechukua njia tofauti," aliongeza.
Mama huyo wa mabinti wawili katika mahojiano ya awali alieleza kwa hisia za uchungu jinsi wakwe zangu walinunia uvaaji wake na matendo yake kama mwanamke aliyeolewa.
Licha ya kuwa muongeaji sana kuhusu penzi lake lililogonga mwamba kwa Kenrazy, kwa upande wake Kenrazy huwa adimu sana kuzungumzia kilichojiri.
Wawili hao walipatana kama wasanii na kuanza mapenzi yao wakiwa chini ya lebo ya Grandpa Records.