Muigizaji Brian Hausa, aliyejizolea umaarufu katka kipindi cha Maria kwenye runinga ya Citizen kati ya mwaka 2019 na 2021 akicheza kama Luwi Hausa amewaacha mashabiki wengi wakiwa na hofu kuhusu hali yake ya kiakili.
Hii ni baada ya muigizaji huyo kuchapisha video akizungumza kwa hisia kali kuhusu mwisho wa maisha, akisisitiza kwamba amefika mwisho na hawezi tena kuendelea.
“Maisha ni mwisho kwayo yenyewe, na swali pekee kuhusu kama yana faida kuendelea kuyaishi ni kama umetosheka na raha zake,” alinukuu video hiyo.
Katika video hiyo ya sekunde chache, Luwi Hausa alionekana akizungumza baina ya machozi, bila kufafanua haswa nini alikuwa anamaanisha kuchoka kuendelea kukifanya.
“Imekuwa ni muda kidogo na imenichukua muda pia kujitokeza tu na jambo lililopo ni kwamba siwezi kuendelea kufanya hivi tena. Hii imezidi na ndivyo ilivyo. Uchungu… siwezi, ni kama siwezi kufanya hili tena, siwezi tu,” Brian Ogana alizungumza kwa hisia katika video hiyo.
Ujumbe huu wa hofu uliwaacha wengi kwenye njia panda wasiweze kujua ni kipi kinamsibu kijana huyo, huku wengine wakitoa wito kwa walioko karibu naye kumuangalia na kutaarifu mashabiki wake kuhusu hali yake.
Tazama hapa video hiyo;