Msanii na mchungaji Size 8 amenyoosha maelezo yake kamili kuhusu wasifu wake katika tasnia ya kueneza injili.
Akizungumza na Obinna, Size 8 alibainisha kwamba yeye wakati mwingi angependa kutambuliwa kama mwinjilisti na wala si nabii kama ambavyo Obinna alijaribu kumtambua.
“Mimi si nabii, acha niseme mimi ni mwinjilisti. Kwa sababu napenda kueneza injili ya Yesu Kristo. Ndio maana kila mahali ninakoenda, huwa siambii watu kwa sababu mimi ni mkamilifu, ninazungumza kumhusu Yesu kwa sababu zawadi ya maana ambayo naweza nikakupa kama binadamu ni Yesu Kristo ambaye amenipa Imani,” alisema.
Msanii huyo alieleza sababu ya kutojikita zaidi katika kufanya muziki zaidi kama siku za nyuma.
Alisema kwamba aliamua kupunguza kasi ya kufanya muziki baada ya afya yake kumvuruga.
“Mwili wangu kidogo ulikataa,” aliongeza.
Awali, mama huyo wa watoto wawili licha ya kudai kutengana na mpenzi wake Dj Mo, alimsifia baba huyo wa watoto wake akisema kuwa ni baba bora licha ya kulelewa bila baba.
Size 8 alisema kuwa licha ya Mo kulelewa na mama yake pekee na kukosa nafasi ya baba katika maisha yake katika maisha yake ya utotoni, amejitahidi sana kuwa baba bora kwa wanawe kwani anatekeleza majukumu yake kama baba ambaye mwenyewe hakumuona.