"Uza nyumba yako, gari au figo!" Vybz Kartel atoa maelezo ya shoo ya kwanza baada ya kutoka jela

"Uza nyumba yako, uza gari lako ikiwezekana, au uuze figo yako nchini China," Vybz alisema.

Muhtasari

•Akizungumza katika mahojiano ya hivi majuzi, Vybz alifichua kwamba atafanya tamasha kubwa mwishoni mwa mwaka huu.

•Vybz amewataka mashabiki wake kutafuta na kuweka pesa ili wawe tayari kununua tikiti pindi zitakapoanza kuuzwa.

Vybz Kartel
Image: HISANI

Staa wa dancehall kutoka Jamaica ambaye hivi majuzi aliachiliwa kutoka jela, Adidja Palmer almaarufu Vybz Kartel, amethibitisha kuwa atarudi tena jukwaani hivi karibuni.

Akizungumza katika mahojiano ya hivi majuzi nchini Jamaica, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 48 alifichua kwamba atafanya tamasha kubwa mwishoni mwa mwaka huu.

Katika maandalizi ya tamasha hilo, aliwataka mashabiki wake kutafuta na kuweka pesa ili wawe tayari kununua tikiti pindi zitakapoanza kuuzwa.

“Shoo ya kwanza itakuwa Desemba. Sitatoa tarehe rasmi lakini anza kuweka pesa zako,” Vybz Kartel alisema kwenye mahojiano hayo.

Aliongeza, "Uza nyumba yako, uza gari lako ikiwezekana, au uuze figo yako nchini China."

Hivi majuzi, msanii huyo anayeshabikiwa na mamilioni ya vijana dunianiMwimbaji huyo alikuwa amethibitisha kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba Kenya ni moja wapo ya nchi ambazo anapanga kufanya ziara za kimuziki.  

Tangazo hilo siku chache baada ya staa huyo wa dancehall kuachiliwa kutoka jela ambapo alikuwa amefungwa kwa takriban miaka kumi na tatu.

Mnamo Julai 31, 2024, Kartel na washtakiwa wenzake watatu waliachiliwa kutoka gerezani kwa uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Rufaa ya Jamaica.

Mashabiki kutoka kote ulimwenguni walisherehekea kuona mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 48 akiungana na familia yake na marafiki baada ya kufungwa kwa takriban miaka 13. Amekuwa gerezani tangu 2011 baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya Clive "Lizard" Williams.

Wakati wa kuachiliwa kwake, alikutana na umati wa wafuasi ambao walimshangilia wakati akitoka gerezani. Hata hivyo, alikuwa amevaa miwani ya jua na kanga ili kuficha uso wake.

Hata hivyo baadaye, picha na video za wazi za msanii huyo ziliibuka zikionyesha jinsi uso na shingo yake ilivyovimba, jambo ambalo lilizua wasiwasi miongoni mwa mashabiki wake.

Inaripotiwa kuwa nyota huyo wa dancehall amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Graves na ugonjwa mbaya wa moyo, ambao ulizingatiwa wakati wa kuachiliwa kwake.

 Wakati wa uamuzi huo, iliamuliwa kwamba ugonjwa wa Graves ulitoa hatari ya wazi na ya sasa kwa ustawi wa Vybz, ambayo inaonekana iliimarisha uamuzi wa kuachiliwa kwake.

Ugonjwa wa Graves, ni hali ya mfumo wa kinga ambayo husababisha mwili kutoa homoni nyingi za tezi, kulingana na Kliniki ya Mayo. Ugonjwa huo unaweza kusababisha ugonjwa wa jicho la tezi, unaonyeshwa na macho makali.

Zaidi ya hayo, Vybz pia anaugua ugonjwa wa moyo.