Vera Sidika alaani aliyehariri jina lake kwenye Wikipedia na kumuita ‘Vera Shikwekwe’

Maelezo ya wasifu wake kwenye Wikipedia yanamtambua kama Vera Shikwekwe, mwanasosholaiti ambaye alianza kuigiza kwenye kipindi cha uhalisia kwenye runinga cha Nairobi Diaries mwaka wa 2015.

Muhtasari

• Mama huyo wa watoto wawili alimlaani aliyehariri jina lake kaitka mtandao huo akisisitiza hajui Shikwekwe ni nani.

VERA SIDIKA.
VERA SIDIKA.

Mwanasosholaiti Vera Sidika ambaye yuko kaitka ziara ya kujivinjari nchini Jamaika ameonyesha kukasirishwa kwake na mtu aliyehariri jina lake kwenye jukwaa la Wikipedia.

Vera Sidika alisema kwamba aligundua kuna mtu aliyekwenda katika jukwaa hilo la kutoa maelezo kuhusu vitu mbalimbali na kubadilisha maelezo kumhusu.

Alisema kwamba jina lake lilihaririwa na mtu Fulani kutoka Vera Sidika na kuitwa Vera Shikwekwe, jina ambalo amekuwa akihusishwa kuwa ni lake la ukoo japo amekuwa alikikataa vikali.

Mama huyo wa watoto wawili alimlaani aliyehariri jina lake kaitka mtandao huo akisisitiza hajui Shikwekwe ni nani.

“Yeyote aliyehariri jina langu kwenye Wikipendia anaelekea kuzimu. Nani ndiye Shikwekwe?” alihoji.

Maelezo ya wasifu wake kwenye Wikipedia yanamtambua kama Vera Shikwekwe, mwanasosholaiti ambaye alianza kuigiza kwenye kipindi cha uhalisia kwenye runinga cha Nairobi Diaries mwaka wa 2015.

Kando na hayo, Sidika alifichua kwamba kuna watu tofauti tofauti ambao wamekuwa wakionesha nia ya kumtunuku zawadi za hela kutokana na urembo wake licha ya kwamba hawajuani, hawajawahi kutana na haitakuja kutokea wao kukutana.

“Watu mbalimbali wamekuwa wakitaka kunitumia pesa takribani kila siku, kwa sababu tu niko mrembo. Hawajawahi kukutana nami, hawatawahi, hawana namba yangu, nyinyi wote ni watu wazuri sana,” alisema.