Mcheza santuri, DJ Mo amefichua siri ya kudumu kwa uhusiano wake na mkewe, Size 8 zaidi ya miaka 10 licha ya wiki mbili zilizopita Size 8 kudai kwamba wameachna.
Akizungumza kwenye kipindi cha Love in the Wild kwenye runinga ya TV47, Dj Mo alifichua kwamba yeye waliketi chini na wakaelewana na mkewe kwamba katika ndoa yao, hakuna atakayejishughulisha na simu ya mwenzake.
“Sisi tushawahi kusikilizana, mimi nishawahi mwambia kaa tu na yako, kwa sababu wakati mwingine kuna kutoelewana kwingi. Unaweza kuwa umekaa tu hivi halafu mtu apige tu simu, hivyo unajipata unatakikata kujieleza zaidi; huyo ni nani, mnafanya nini.. .hivyo tulikubaliana ikae,” alisema.
Dj Mo alisema kwamba anajua kila wanandoa k una maelewano katika ndoa yao lakini akasisitiza kwamba katika ndoa yake na Size 8, jambo moja ambalo walilitafutia mwafaka ni kuhusu simu.
Baba huyo wa watoto wawili alitoa sababu ya uamuzi wa maelewano hayo.
“Naamini kila wanandoa kuna venye wameakubaliana, lakini mimi na mke wangu tulikubaliana simu yake anakaa nayo na mimi nakaa na yangu si kwa sababu ya kitu chochote au kuna kitu mtu anaficha ila tu ni kwa sababu ya kujaribu kukwepa kujieleza kwingi,” DJ Mo alisema.
Hata hivyo, katika kipindi hicho, Dj Mo bado walikuwa na mkewe Size 8 licha ya msanii huyo ambaye pia ni mchungaji kufichua kwamba alikuwa ameanza safari ya maisha bila mume.