Vybz Kartel adokeza nia yake ya kuingia kwenye siasa, kuwania ubunge Jamaika

Kwa mujibu wa kituo kimoja cha redio nchini humo kwa jin Natiowide Radio, Kartel anasema eneo bunge lake la uchaguzi litakuwa Kusini mwa St. Catherine ambalo linawakilishwa na Fitz Jackson wa chama cha PNP tangu 1994.

Muhtasari

• Kartel, ambaye jina lake ni Adidja Palmer, alitoa maoni hayo alipokuwa akizungumza kwenye moja kwa moja ya TikTok na wakili wake, Isat Buchanan.

VYBZ KARTEL
VYBZ KARTEL
Image: HISANI

Msanii wa dancehall aliyeachiliwa huru Vybz Kartel amedokeza uwezekano wa kujitosa kwenye siasa na kuwania kama mnunge.

Akuzungumza kwenye mahojiano yake ya kwanza, wiki mbili baada ya kuondoka jela alikohudumia kifungo cha miaka 13, Kartel alisema hali ya sasa ya jamii ya Jamaika inaweza kumfanya kugombea Ubunge.

Kartel, ambaye jina lake ni Adidja Palmer, alitoa maoni hayo alipokuwa akizungumza kwenye moja kwa moja ya TikTok na wakili wake, Isat Buchanan.

Kwa mujibu wa kituo kimoja cha redio nchini humo kwa jin Natiowide Radio, Kartel anasema eneo bunge lake la uchaguzi litakuwa Kusini mwa St. Catherine ambalo linawakilishwa na Fitz Jackson wa chama cha PNP tangu 1994.

"Tutaona," nyota wa dancehall Vybz Kartel alisema, "Ingia kama mimi naenda tu kuwa mbunge kwa sababu kuzungumza wakati fulani hakukupeleki mahali, wakati mwingine unahusika, lakini tutaona," alisema.

Pendekezo la kuwa mbunge lilikuja huku Kartel akilalamikia dhuluma mbalimbali katika jamii. Kartel anasema ukosoaji wake hauelekezwi kwa chama chochote.

Kartel, 48, ambaye ameachiliwa kutoka gerezani kwa wiki mbili sasa, amekuwa akigonga vichwa vya habari ndani na nje ya nchi hiyo ya Karibia tangu kuachiliwa kwake.

Ingawa hajafanya uamuzi wa uhakika, alithibitisha na wakili wake Isat, ambaye alisema, "Hilo ni wazo, unajua," kwa kusema, "Najua, na mimi ni mbaya, lakini tutaona."