Zari na Shakib waripotiwa kukwaruzana kisa Diamond kutembelea wanawe bila taarifa (video)

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari za burudani, ujio wa Diamond bila taarifa nyumbani kwa Zari kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Tiffah kulimkera Shakib ambaye alimtuhumu Zari kwamba bado anampenda Diamond.

Muhtasari

• “Alikuwa mwendawazimu, akanihoji kwa nini sikumwambia Diamond anakuja. Alisema, labda bado ninampenda baba wa watoto wangu,” Zari alisimulia kwenye video hiyo.

SHAKIB NA ZARI WAKWARUZANA KISA DIAMOND
SHAKIB NA ZARI WAKWARUZANA KISA DIAMOND
Image: HISANI

Zari na mumewe Shakib wameripotiwa kukwaruzana tena baada ya babydaddy wa Zari, Diamond Platnumz kutembelea wanawe Afrika Kusini bila taarifa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya bintiye, Tiffah.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari za burudani, ujio wa Diamond bila taarifa nyumbani kwa Zari kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Tiffah kulimkera Shakib ambaye alimtuhumu Zari kwamba bado anampenda Diamond.

Katika video kwenye TikTok, Zari alijitetea vikali akisema kwamba hata yeye hakuwa anajua kama Diamond alikuwa amepanga kuwatembelea bila kutoa taarifa, akisema jambo hilo lilimkera mumewe, Shakib.

“Alikuwa mwendawazimu, akanihoji kwa nini sikumwambia Diamond anakuja. Alisema, labda bado ninampenda baba wa watoto wangu,” Zari alisimulia kwenye video hiyo.

Hata hivyo, Zari alieleza kuwa hakufahamu mpango wa Diamond kutembelea, ambao alisema ulipangwa na watu wanaoishi nyumbani kwake.

“Diamond Platnumz Wallahi hakuniambia kwamba anakuja,” Zari alisisitiza akisema kwamba muda wote aikuwa anamtuhumu kwa kutopokea simu zake kutokana na kuwa na ukaribu muda wote na mumewe, Shakib.

Kutokana na hilo, Zari alisema aliamua kumpa Diamond namba ya simu ya moja ya manyikazi wake ili kuwasiliana naye kuhusu masuala ya watoto, kwa sababu Shakib alikuwa haoni vizuri yeye kuendelea kuzungumza na Diamond moja kwa moja.

Anashikilia, hata hivyo, kwamba hana njia ya kumzuia ex wake kuona watoto wake.

Alieleza kuwa Diamond bado hutoa mahitaji yote ya watoto wake na hata alituma pesa kusaidia maandalizi ya siku ya kuzaliwa.

Hata kwenye party hiyo, Zari anasema hakuweza kukunja uso wala kumpuuza Diamond, “kwa sababu hawa ni watoto wake, na mimi ni mama yao.”