• Mashabiki wa mtangazaji huyo wa kipindi cha Bustani katika Radio Jambo waliungana naye kutuma jumbe za heri njema kwa bintiye anapokaribia kuondokea utineja.
Mtangazaji wa stesheni ya Radio Jambo, Massawe Japanni amesherehekea bintiye wa kwanza kufikisha umri wa miaka 17.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Japanni alichapisha msururu wa picha za mwanawe huyo tangu akiwa mdogo na kusherehekea safari ya kupendeza ya maisha ambayo wameikwea pamoja kwa karibia miongo miwili sasa.
“Miaka kumi na saba ya kupendeza❤️ Happy birthday binti yangu,” mama huyo wa mabinti watatu warembo aliandika.
Mashabiki wa mtangazaji huyo wa kipindi cha Bustani katika Radio Jambo waliungana naye kutuma jumbe za heri njema kwa bintiye anapokaribia kuondokea utineja.
“Huyu si nilimbeba na kumuona hospitali? 17 vipi??????” Mtangazaji Tallia Oyando alistaajabu.
“Imani ana miaka 17??? Furaha zaidi ya siku ya kuzaliwa, Imani kutoka kwa Nana na mimi❤️"”Ngash Kendy.
" Ohhh mtu wangu wa kibinafsi ... na anaweza kujua na kutumia sauti yake mapema na kila wakati. Kwa siku nyingi zaidi zilizojaa kicheko,” Anne Mawathe.