• Mama huyo wa watoto 2 alifichua kwamba binti yake na umri wake mdogo hivyo, tayari ameacha kulia wakati wa kuenda shule.
Mwanamitindo Amber Ray ameonyesha furaha yake baada ya bintiye mwenye umri wa miezi 15 tu kuanza kuzoea maisha ya kuenda shuleni.
Kupitia insta story yake, Amber Ray alichapisha picha ya binti yake akiwa kando la gari la kifahari aina ya Range Rover akisema kwamba walikuwa wanasubiria gari la kumpeleka shuleni.
Mama huyo wa watoto 2 alifichua kwamba binti yake na umri wake mdogo hivyo, tayari ameacha kulia wakati wa kuenda shule.
“Mwanangu yuko tayari kuenda shule, angalia jinsi ana hamu ya kusubiri gari la kumpeleka shuleni. Yaani sasa halii tena,” Amber Ray alisema h uku akihoji ni nini ambacho shule ya chekechea anayosoma bintiye wanampa.
Amber Ray alijifungua mtoto huyo kwa jina Africanah mwezi Mei mwaka jana na hivi majuzi katika mahojiano, alieleza kwa nini aliamua kumpeleka shuleni hata kabla ya kufikisha umri wa miaka 2.
“Najua ni mdogo lakini msichokifahamu ni kwamba yule binti ni mwenye akili nyingi. Ukipata nafasi ya kuketi na Africanah hapa huwezi hata fikiria kwamba ana umri wa mwaka mmoja na miezi 3. Unaweza dhani amefika umri wa zaidi ya miaka 2 ukisikia vile vitu anafanya, anasikia… nahisi kwamba kwetu sisi tukikaa naye nyumbani itakuwa kama tunamshusha chini,” Ray alisema.