logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Meneja wa Zari kwa Shakib: Acha kulia-lia kama mtoto, muite Diamond mpigane ngumu!

Anthony alisema kwamba amekutana na Shakib mara nyingi na anaweza kusema kwamba kijana huyo hayuko serious.

image
na Davis Ojiambo

Burudani14 August 2024 - 10:32

Muhtasari


  • • Anthony alisema kwamba amekutana na Shakib mara nyingi na anaweza kusema kwamba kijana huyo hayuko serious.
ZARI NA MENEJA WAKE

Meneja wa mjasiriamali Zari Hassan, Galston Anthony amevunja kimya chake kuhusu zogo linaloendelea baina ya bosi wake na mpenziwe, Shakib Lutaaya Cham.

Anthony kupitia Instagram, alichapisha video akimzomea Shakib kwa kile alisema kwamba ameonyesha hulka ya utoto kudai Zari anamsaliti kimapenzi kwa kuonekana na mpenzi wake wa zamani ambaye pia ni baba wanawe, Diamond Platnumz.

Meneja huyoo alisema kuwa kwa wanaume wote, Shakib hafai kulalamika au kuonyesha hofu ya kusalitiwa kimapenzi na Zari kutokana na jinsi ambavyo Zari amekuwa akimheshimu kama mpenzi wake wa pekee.

“Shakib Shakib Shakib! Angalia kitu imenipelekea kufanya. Nimelazimika kufanya hii video kwa ajili yako. Zari amejijengea jina kibinafsi ya wewe bado hujajijengea. Daimond anajua kila mara atakuburuza kwa sababu huna jina mitandaoni, pili kwa sababu umechaguliwa na mtu maarufu katika bara zima na unaanza kuhisi kusalitiwa,” Anthony alisema.

“Ningependa kukwambia kwamba unastahili kujitokeza na kukoma kuhisi kama unasalitiwa, na anza kujijengea jina lako. Na kama unahisi Diamond anakukosea heshima si umwalike muingie kwenye mduara mzichape,” alisema.

Anthony alisema kwamba amekutana na Shakib mara nyingi na anaweza kusema kwamba kijana huyo hayuko serious.

“Sasa nahisi hauko serious, nimekutana na wewe mara nyingi n nimekupa ushauri mara dufu lakini ni kama hautilii maanani. Unataka nifanye nini? Ninyamaze? Sasa Zari atakuwa anaongelelea mitandaoni, yeye ni supastaa anaweza akafaya chochote anataka, ako katika sehemu kwamba chochote kinatokea mitandaoni anaweza kukimudu na wewe ungestahili kumudu maisha ya faragha ya ndoa,” alishauri.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved