Rick Ross achukua mtandaoni kulalamika rafiki anayeishi naye kwake kulala hadi 11:30am

“Unaona ninazungumza kuhusu kulala hadi kuchelewa. Niligundua kuwa nilikuwa na mtu chini ya paa moja na mimi, na ni 11:30am? Bado amelala. Hilo haliwezi kuvumiliwa." Ross alisema.

Muhtasari

• Alianza kwa kuwashauri wafuasi wake umuhimu wa kuanza siku alfajiri mapema kabla ya kugundua kuwa rafiki yake alikuwa bado anang’orota kitandani majira ya saa tano.

RICK ROSS
RICK ROSS
Image: HISANI

Msanii wa Marekani Rick Ross amezua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kuchapisha video akilalamika vikali kuhusu hulka isiyo ya kupendeza ya rafiki yake ambaye anaishi kaitka jumba lake la kifahari.

Katika video hiyo, Rossey – kama anavyojiita kwa madoidoi, alionyesha kuchukuzwa na tabia ya mmoja wa marafiki zake ambaye anaishi naye kaitka jumba lake la kifahari kulala hadi saa tano na nusu mchana.

Alianza kwa kuwashauri wafuasi wake umuhimu wa kuanza siku alfajiri mapema kabla ya kugundua kuwa rafiki yake alikuwa bado anang’orota kitandani majira ya saa tano.

“Unaona ninazungumza kuhusu kulala hadi kuchelewa. Niligundua kuwa nilikuwa na mtu chini ya paa moja na mimi, na ni 11:30am? Bado amelala. Hilo haliwezi kuvumiliwa. Lazima nifanye jambo kuhusu hilo, uko tayari? Njoo nami," Ross alisema kwenye hadithi ya Instagram.

Baada ya kuingia chumbani, rafiki yake mwingine alimletea kipeperushi cha majani na kumpulizia rafiki yake aliyekuwa amelala usoni. Maskini jamaa yule aligutuka kutoka usingizini aliwa amechanganyikiwa huku Rossey na wenzake wakimcheka.

"Huwezi kuwa unalala kwa mtu mwenye pesa. Itamuumiza mtu mmoja tu,” alihitimisha Rick Ross baada ya kumtania rafiki yake.

Hii hapa video hiyo;