Shakib Cham aanza safari ya kujfunza kuwa mtaalamu katika upiganaji ngumi za kulipwa

". Ningependa kupigana na wanabondia au yeyote ambaye atakuwa na nia ya kupigana name au kuingia kwenye ulingo na mimi,” Shakib alisema.

shakib
shakib
Image: YouTube

Mume wa mwanasosholaiti Zari Hassan, Shakib Cham Lutaaya amethibitisha kujitosa kwenye ulingo wa bondia ili kupata mafunzo ya kuwa mtaalamu katika upiganaji ngumi.

Akizungumza kupitia kwa chaneli yake ya YouTube, Shakib alisema kwamba kwa sasa ameanza safari ya kujifunza ngumi na anatarajia siku si nyingi kutoka leo kuingia katika pambano moja la ngumi za kulipwa.

“Kama ambavyo nimekuwa nikisema, nimekuwa nikijenga taaluma yangu kaitka ndondi. Hivyo hivi karibuni au mbeleni huko nitakuwa na pambano moja la kulipwa. Ningependa kupigana na wanabondia au yeyote ambaye atakuwa na nia ya kupigana name au kuingia kwenye ulingo na mimi,” Shakib alisema.

Hata hivyo, alisisitiza kwamba yeye hataki kushiriki kaitka mchezo wa mieleka bali tu kaitka kupigana ngumi za kawaida tu basi.

“Ni mchezo wa ngumi tu, sipendi kickboxing au UFC au aina nyingine yoyote, napenda tu ndondi. Tayari mimi najiona kama nishakuwa mwanabondia mtaalamu kwa sababu nimekuwa nikipigana na wataalamu katika ngumi,” alisema.

Kijana huyo alifichua kwamba ametoka katika familia ya wanabondia sema tu ni yeye mwenyewe hakutaka kujihusisha kwenye ngumi miaka ya nyuma lakini ndoto hiyo inamjia sasa.

Alisema kuwa akiwa mdogo alikuwa anajifunza kuwa bondia lakini akafika mahali akaachana na mchezo huo.

“Nilikuwa nafanya boxing kitambo nikiwa mdogo, lakini wakati nilikuwa mkubwa, nilikata tamaa na boxing kwa sababu nilitaka vitu vingine vikubwa.”