“Upendo wa familia ndio baraka kuu ya maisha” – Nadia Mukami

Msanii huyo alisisitiza kwamba si lazima uwe na uhusiano wa kiukoo na mtu ili kumtambua kama familia yako, bali kitendo cha upendo pekee ni ithibati tosha ya kuita mtu miongoni mwa wanafamilia wako.

NADIA MUKAMI NA ARROW BWOY NA MWANAO.
NADIA MUKAMI NA ARROW BWOY NA MWANAO.
Image: INSTAGRAM

Malkia ya muziki wa Kenya, Nadia Mukami amezungumzia kuhusu umuhimu wa familia, akichappisha picha za pamoja za familia yake; yeye mumewe na mwanao Kai.

Nadia alifafanua kwamba familia ndio watu pekee ambao wanakuelewa wakati unapitia hali zote, kuwa na mtu yeyote ambaye unaweza penda huyo tayari anakuwa familia yako.

Msanii huyo alisisitiza kwamba si lazima uwe na uhusiano wa kiukoo na mtu ili kumtambua kama familia yako, bali kitendo cha upendo pekee ni ithibati tosha ya kuita mtu miongoni mwa wanafamilia wako.

“Kuwa na mahali pa kwenda ni nyumbani. Kuwa na mtu wa kumpenda ni familia. Kuwa na vyote viwili ni baraka. Familia haijafafanuliwa na jeni zetu, inajengwa na kudumishwa kwa njia ya upendo,” alisema.

Kwa mujibu wa Mukami, kiunganishi cha familia si lazima kiwe kuhusu damu, bali mtu anayekupa heshima na furaha pia huchangia mtu kujihisi kuwa ni mmoja wa familia yako.

“Uhusiano unaounganisha familia yako ya kweli si wa damu, bali wa heshima na furaha katika maisha ya kila mmoja wao. Upendo wa familia ni baraka kuu ya maisha,” aliongeza.

Nadia na Arrow Bwoy wamekuwa moja ya kielelezo bora cha familia yenye heshima na upendo, huku wakifanya kazi pamoja kwenye biashara na hata katika Sanaa pia.