TikToker Faustine Lipuku Lukale maarufu kama Baba Talisha ameadhimisha miaka 4 tangu kifo cha ghafla cha mpenziwe.
Kupitia Instagram, Baba Talisha alichapisha picha ya mrembo huyo aliyemuacha na binti mmoja akisema kwamba alifariki na nguvu zake zote kama mwanamume.
Baba Talisha alisema kwamba akiwa naye, alikuwa anajiona kama mwanamume mwenye nguvu lakini baada ya kuondoka kwake, amekuja kugundua kuwa hakuwa na nguvu zozote bali ni kutokana na uwepo wake ambao ulikuwa unampa nguvu za kujidai.
“Leo umetimiza miaka 4 kamili tangu ulipoondoka 🕊Nilijiona kama mwanaume hodari na mwenye uwezo- lakini sasa natambua kuwa nguvu na uwezo ulitoka kwako na nilikuwa mwanaume aliyebahatika kuolewa na mwanamke mwenye nguvu na uwezo. Sasa kwa kuwa nimepoteza chanzo hicho, nimekuwa dhaifu na siwezi kuishi maisha yenye tija,” Baba Talisha alisema.
TikTok huyo baba wa binti mmoja alifichua kwamba hajawahi kuwa mtu wa kuamini katika miujiza lakni jambo moja ambalo anaamini lilitokea kwake kimiujiza ni kumpata mpenzi wake.
“Sijawahi kuwa muumini wa miujiza, kama unavyojua. Lakini nikitazama nyuma, kupata njia yangu kwako haikuwa kitu kingine kando na muujiza - na ningepingana na mtu yeyote anayesema sivyo. Najua ni upuuzi kuamini kwamba muujiza mwingine ungenirudisha kwako- lakini nachagua kuamini; coz otherwise maisha yangu hayana maana yoyote. Lala lala Malkia,” aliongeza.
Baba Talisha katika mahojiano ya awali aliwahi funguka jinsi ajali hiyo ilitokea, akisema ni tukio lililojiri kwa haraka na ghafla mno.