Binti wa Mike Sonko adai watu wanauza na kununua namba yake ya simu kwa Sh2,500

Binti huyo wa Sonko anaamika kuwa kwa sasa yuko nchini UIngereza kujiendeleza kimasomo baada ya kufichua kuhusu safari yake mwishoni mwa mwaka jana.

SANDRA MBUVI
SANDRA MBUVI
Image: INSTAGRAM

Sandra Mbuvi, maarufu kama Thickyy Sandra ameshangaza watu mtandaoni baada ya kudai kuna watu wanafanyia biashara namba yake ya simu.

Binti huyo mdogo wa aliyekuwa gavana wa Nairobi, Mike Sonko aliandika kupitia Instagram yake kwamba amegundua kuna watu wanauza na kununua namba yake ya siku kwa shilingi 2,500.

Alisema kwamba wengi wanaonunua namba hiyo kutoka kwa walle wenye wako nayo baadae huingia kaitka faragha zake na kumuandikia ujumbe kwamba walinunua namba yake ili kufanya mazungumzo naye.

Hata hivyo, binti huyo mkwasi alikula yamini kwamba hatojibu jumbe zozote za wale wanaokiri kununua namba yake ili kupata mawasiliano naye.

“Niambieni ni kwa nini nyinyi wote mnauza na kununua namba yangu? Halafu mnakula kulalamika kwangu eti mlinunua namba yangu ya simu kwa Sh2,500, hiyo ni nini? Mkiwa mnajua kabisa kwamba siwezi kuwajibu,” aliandika.

thickyy sandra,
thickyy sandra,

Binti huyo wa Sonko anaamika kuwa kwa sasa yuko nchini UIngereza kujiendeleza kimasomo baada ya kufichua kuhusu safari yake mwishoni mwa mwaka jana.