• Miezi kadhaa baadae, Salasya alishinda uchaguzi wa Agosti 8, 2022 kama mbunge wa Mumias Mashariki na maisha yake sasa hivi yamebadilika.
Mbunge wa Mumias Mashariki, Peter Salasya amechapisha picha moja kutoka siu zake za mihangaiko kabla ya kuwa mbunge.
Salasya katika picha hiyo anaonekana mnyonge na kufichua kwamba hakuwa amelewa licha ya wengi kwenye upande wa kutoa maoni kdhani kwamba alikuwa mlevi wakati wa kupiga picha hiyo.
Alionekana akiwa ameketi kwenye kiti na kando yake akiwa na barakoa na simu na kufichua kuwa hapo alikuwa ameenda hospitalini 2021 baada ya kushambuliwa na watu aliowaita kuwa wahuni waliotumwa na mwanasiasa mmoja.
“Hapa sikuwa nimelewa ilikuwa 2021 nimeundwa vilivyo na goons wa [jina limebanwa]. Saa nane mchana pale cereals Maraba Kakamega town kama umbwa,” Salasya alisema.
Mbunge huyo alishagaza wengi kwa kufichua kwamba baada ya kufika hospitalini kwa ajili ya matibabu, mambo yalimgeukia tena kwa kutuhumiwa kuwa mwizi wa simu kaitka hospitali hiyo, akisema kuwa ni kutokana na muonekano wake wa kutia huruma.
“Sasa I had gone to hospital pale Kakamega CGH tena wakaniwekea nilikuwa nimeiba simu. Haki nilitesaka nikifikiria tu mashida nilipitia husema wacha tu God aitwe God. Sometimes frustrations we go through inafungua mlango mwingine,” alisema.
Miezi kadhaa baadae, Salasya alishinda uchaguzi wa Agosti 8, 2022 kama mbunge wa Mumias Mashariki na maisha yake sasa hivi yamebadilika.