Simple Boy na Dem wa FB wakichumbiana wana uwezo wa kuwa ‘power couple’ – Director Trevor

Alisema kwamba Stevo Simple Boy na Dem wa Facebook wakiweza kuchumbiana tu na kuwa wapenzi, penzi lao litakuwa la kupigiwa mfano na wengi.

Muhtasari

• Alisema kwamba Stevo Simple Boy na Dem wa Facebook wakiweza kuchumbiana tu na kuwa wapenzi, penzi lao litakuwa la kupigiwa mfano na wengi.

DEM WA FB NA STEVO SIMPLE BOY.
DEM WA FB NA STEVO SIMPLE BOY.
Image: Facebook

Director Trevor amewashauri msanii Stevo Simple Boy na mchekeshaji Dem wa Facebook kufikiria suala la kuingia katika mahusiano.

Kwa mujibu wa Trevor, wawili hao wanaweza ungana pamoja na kufaidi pakubwa kutokana na umaarufu wao kaitka mitandao ya kijamii.

Alisema kwamba Stevo Simple Boy na Dem wa Facebook wakiweza kuchumbiana tu na kuwa wapenzi, penzi lao litakuwa la kupigiwa mfano na wengi.

“Stevo Simple Boy na Dem wa Facebook wakiweza chumbiana wanaweza kuwa wachumba wa nguvu sana,” Director Trevor aliandika katika picha ya pamoja na wawili hao.

Stevo na Dem wa FB ni wasanii wawili ambao wamezungumziwa mara nyingi kaitka mitandao ya kijamii kwa njia hasi, kutokana na mionekano yao wakiitwa ‘vienyeji’.

Msanii huyo wa Freshi Barida amekuwa akisuasua katika suala la maisha ya mapenzi, miaka miwili tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake, Pritty Vishy.

Kwa upande wake, Dem wa Facebook ambaye amepata umaarufu hivi majuzi hayawahi weka wazi maisha yake ya kimapenzi, kwa wakati mmoja akisema kwamba hayuko tayari kujihusisha kimapenzi na mtu yeyote hadi pale atakapotimiza ndoto za kuwaweka wazazi wake katika maisha mazuri.