logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Simple Boy atangaza kwa furaha kusafiri nje ya nchi kwa mara ya kwanza maishani mwake

“Hayawi hayawi huwa. Kwa mara ya kwanza nasafiri nje ya nchi na msanii wangu mkali Machabe,” Stevo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 August 2024 - 13:10

Muhtasari


  • •   “Wafuasi wangu ahsanteni kwa sapoti mmenipa huu mwaka, tuzidi hivyo hivyo na mambo itakuwa mwake mwake,” alishukuru.
STEVO SIMPLE BOY

Rapa Stevo Simple Boy ametangaza kwa furaha kwamba kwa mara ya kwanza katika maisha yake, anatarajia kusafiri nje ya nchi.

Msanii huyo wa Freshi Barida alitoa taarifa hizi kupitia insta story yake akisema kwamba ana furaha isiyo kifani kutangaza taarifa hizo kwa mashabiki wake.

Msanii huyo alifichua kwamba atasafiri na msanii aliyedai kumsaini kwa jina Machabe bila kufichua nchi wanakokwenda.

“Hayawi hayawi huwa. Kwa mara ya kwanza nasafiri nje ya nchi na msanii wangu mkali Machabe,” Stevo Simple Boy alisema.

Msanii huyo aliwashukuru mashabiki wake ambao wamekuwa wakimpa sapoti tangia mwaka 2019 alipochipuka na wimbo wa Mihadarati.

“Wafuasi wangu ahsanteni kwa sapoti mmenipa huu mwaka, tuzidi hivyo hivyo na mambo itakuwa mwake mwake,” alishukuru.

Msanii huyo ameonekana kupata mwamko mpya katika siku za hivi mauzi, miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekuwa meneja wake.

Wiki iliyopita, alizua gumzo mitandaoni akidai kwamba hawezi kubali kuanya kolabo na gwiji wa bongo fleva, Diamond Platnumz ikiwa hatomlipa milioni 20 za Kenya kwa ajili ya hilo.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved