• “Wafuasi wangu ahsanteni kwa sapoti mmenipa huu mwaka, tuzidi hivyo hivyo na mambo itakuwa mwake mwake,” alishukuru.
Rapa Stevo Simple Boy ametangaza kwa furaha kwamba kwa mara ya kwanza katika maisha yake, anatarajia kusafiri nje ya nchi.
Msanii huyo wa Freshi Barida alitoa taarifa hizi kupitia insta story yake akisema kwamba ana furaha isiyo kifani kutangaza taarifa hizo kwa mashabiki wake.
Msanii huyo alifichua kwamba atasafiri na msanii aliyedai kumsaini kwa jina Machabe bila kufichua nchi wanakokwenda.
“Hayawi hayawi huwa. Kwa mara ya kwanza nasafiri nje ya nchi na msanii wangu mkali Machabe,” Stevo Simple Boy alisema.
Msanii huyo aliwashukuru mashabiki wake ambao wamekuwa wakimpa sapoti tangia mwaka 2019 alipochipuka na wimbo wa Mihadarati.
“Wafuasi wangu ahsanteni kwa sapoti mmenipa huu mwaka, tuzidi hivyo hivyo na mambo itakuwa mwake mwake,” alishukuru.
Msanii huyo ameonekana kupata mwamko mpya katika siku za hivi mauzi, miezi kadhaa baada ya kuachana na aliyekuwa meneja wake.
Wiki iliyopita, alizua gumzo mitandaoni akidai kwamba hawezi kubali kuanya kolabo na gwiji wa bongo fleva, Diamond Platnumz ikiwa hatomlipa milioni 20 za Kenya kwa ajili ya hilo.