Mchezaji nguli wa Ureno na Al Nassir, Cristiano Ronaldo amevunja kimya chake saa chache baada ya kuzawadiwa na jukwaa la YouTube kufuatia mafanikio makubwa ndani ya saa chache.
Ronaldo aliarifiwa kuanzisha chaneli yake katika mtandao wa YouTube na ndani ya siku moja, tayari imepata wafuasi zaidi ya milioni 15.
YouTube walimtunuku Ronaldo na Golden Button kwa ufanisi huo mkubwa na Ronaldo aliitaja zawadi hiyo kama ya kupeleka nyumbani kwa wanawe.
Aliwashukuru wafuasi wake katika mtandao wa X na Instagram akitumia neno ‘Siuu’ ambalo ni jina la mtindo wake wa kusherehekea anapofunga bao.
“Ahsante sana kwa SIUUUbscribers,” Ronaldo aliandika na kfichua kupeleka zawadi nyumbani.
Ronaldo alificha nyumbani na kuwaita wanawe kumpokea na zawadi mpya.
“Niko na zawadi mpya, Eva njoo tucheze sisi watatu. Acha tuone nani atashinda,” Ronaldo aliwaonyesha wanawe waliopigwa na butwaa.