• Akijibu, Baba Talisha alikiri kwamba japo huwa anashikilia kinyongo katika roho yake, lakini alishasamehe na kusahau kila kilichotokea.
TikToker Faustine Lipuku Lukaale maarufu kama Baba Talisha kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu zogo kati yake na bibi yake aluyekuwa rafiki yake, marehemu Brian Chira.
Baba Talisha alifunguka kuhusu uhusiano uliopo baina yake na nyanyake Brian Chira kupitia kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram yake na mashabiki wake.
Shabiki mmoja alimuuliza ikiwa amemsamehe nyanyake Brian Chira baada yake kushikana na baadhi ya watumizi wa TikTok na kumburuza matopeni Baba Talisha, siku chache baada ya kumalizika kwa mazishi ya Chira.
Akijibu, Baba Talisha alikiri kwamba japo huwa anashikilia kinyongo katika roho yake, lakini alishasamehe na kusahau kila kilichotokea.
“Nilisonga mbele na maisha yangu. Nilisaidia ninapoweza, nilifanya nilichofanya. Huwa nashikilia kinyongo katika moyo wangu na huwa inanisaidia pakubwa kiakili. Nilisamehe na kusahau, vitu hutokea na sababu maalum, jambo pekee unalopaswa kufanya ni kusimama ngangari na kuomba. Mungu wakati wote atachukua usukani na kukufanyia kila kitu,” alijibu.
Wikendi iliyopita, jamii ya wanatiktok ambao walikuwa marafiki wa Brian Chira walikwenda nyumbani kwake kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa jumba ambalo walimjengea nyanyake Chira.
Jumba hilo lilijengwa kutoka kwa hela ambazo Baba Talisha alisimama kama kiranja na kuzichangisha zaidi ya shilingi milioni 8.
Hata hivyo, Baba Talisha mwenyewe hakuhudhuria hafla hiyo na mmoja alimuliza kwa nini, akasema kwamba anachunga mstari wa maisha yake.