Mwimbaji wa Marekani apoteza wafuasi 25k baada ya kum’unfollow Davido baada ya kumsaidia

Uchunguzi wa kina wa akaunti yake mnamo Ijumaa ulionyesha kuwa wafuasi wake walikuwa wamepungua kutoka 821.9k hadi 796.6k.

Muhtasari

• Baada ya kupoteza wafuasi 25k ndani ya saa 24, Enisa anamfuata tena Davido katika kile kilichoonekana ni kurejesha urafiki uliosambaratika kwa muda.

davido na enisa
davido na enisa

Mwimbaji maarufu wa Marekani kwa jina Enisa amearifiwa kupoteza zaidi ya wafuasi elfu 25 kwenye mtandao wa X baada ya kudaiwa kumkejeli msanii wa Afrobeats, Davido.

Kwa mujibu wa blogu mbalimbali kutoka ukanda wa Afrika Magharibi, Enisa alimkejeli na kisha kusitisha urafiki kwa Davido ambaye aliarifiwa aliwahi mpa msaada mkubwa katika tasnia ya Sanaa.

Kumbuka kwamba mnamo 2021, Davido alishiriki kwenye remix ya wimbo wake "Love Cycle" ili kumsaidia kuungana na mashabiki nchini Nigeria.

Wanigeria katika majukwaa ya mitandao ya kijamii wanamkaribisha vyema na wanaonyesha jinsi wanavyompenda kwa kumpa jina la Eniola.

Uchunguzi wa kina wa akaunti yake mnamo Ijumaa ulionyesha kuwa wafuasi wake walikuwa wamepungua kutoka 821.9k hadi 796.6k.

Wanigeria kama Smallie, mshawishi wa mitandao ya kijamii, na Dapsy pia walimsaidia Enisa kuungana na mashabiki wake wa Nigeria.

Baada ya kupoteza wafuasi 25k ndani ya saa 24, Enisa anamfuata tena Davido katika kile kilichoonekana ni kurejesha urafiki uliosambaratika kwa muda.