Bradley Mtall apata mwaliko kuzuru Dubai

Bradley Mtall ambaye video zake zimekuwa zikisambaa katika mtandao wa kijamii apata afueni baada ya kuomba msaada

Muhtasari

•Bradley Mtall amekabidhiwa mwaliko kwenda ziara Dubai.

• Hii ni siku chache tu baada ya Bradley kualikwa Mombasa na Khushi Motors, ambapo alitia saini ya kuwa balozi wa kampuni hiyo ya kuuza gari.


Bradley Mtall
Bradley Mtall
Image: Bradley Mtall//Facebook

Bradley Marongo, almaarufu "Gen Z Goliath" amealikwa kuzuru Dubai.

Kampuni moja ya  Elektroniki Zam Zam Electronics imemwalika Dubai na kuahidi kulipa hoteli yake na cheti  cha kusafiria.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii, ilionekana kwamba Director Trevor amewasiliana na Zam Zam Electronics na kuwaambia ya kwamba wanashughulikia pasipoti yake na baada ya siku chache itakuwa tayari.

Hii ni siku chache tu baada ya Bradley kualikwa Mombasa na Khushi Motors, ambapo alitia saini ya kuwa balozi wa kampuni hiyo ya kuuza gari.

Matukio ya hivi punde yanaonyesha kubadilika kwa maisha ya Bradley baada ya kupata umaarufu alipoangaziwa na vyombo vya habari nchini.  Alikuwa ameomba kusaidiwa kupata ajira,simu na makazi.

Maombi yake yameanza kuza matunda baada ya kuchaguliwa kuwa  Brand Ambassador wa Khushi Motors na hata kupata mwaliko kutoka kwa Zam Zam Electronics.

Kampuni hii ilimdhamini sana Rango Tenge Tenge mchekeshaji wa umri mdogo kutoka Uganda na kuwa maarufu sana duniani.