• Mchungaji huyo alisisitiza kwamba yeye hawezi kuwakubalia wasichana wake kumletea wajukuu akisema endapo atakubali hilo basi atakuwa hajaokoka.
Mchungaji wa kanisa la Neno Evangelical, James Maina Ng’ang’a amewashangaza waumini wa kanisa lake baada ya kutoa sababu ya kutotaka wajukuu.
Katika moja ya video ambayo imeibuka mitandaoni kutoka kwa moja ya mahubiri yake, Ng’ang’a alisema kwamba kuwalea watoto wa kike ni kibarua cha kipekee na mzazi usipokuwa makini utawapoteza katika raha na anasa za kidunia.
Mchungaji huyo alisema kwamba aliwapa onyo mabinti zake wakati wanakua akiwaulisha wazi kwamba yeyote ambaye angeanya uthubutu wa kupata mimba, basi angeondoka chini ya paa lake.
Ng’ang’a alisema kwamba hilo halikumaanisha kuwatupa bali alikuwa tayari kuwasaidia lakini wakiwa mbali naye, akisema kuwa yeye hakuwa anataka waukuu kwa vile mwenyewe ni mukuu.
“Mimi niliambia wasichana wangu ukizaa ni nje, tutaonaniana kwa salamu za mkono, kama nitakusaidia ni huko huko tu. Lakini kumlelea kwangu azae tena aniletee hapo? Eti wajukuu, wajukuu wa nani? Mimi sitaki wajukuu sababu mimi mwenyewe ni mjukuu,” Ng’ang’a alisema.
Mchungaji huyo alisisitiza kwamba yeye hawezi kuwakubalia wasichana wake kumletea wajukuu akisema endapo atakubali hilo basi atakuwa hajaokoka.
“Pengine hiyo mimi sijaokoka. Hiyo hata sitaokoka, lakini ukienda vizuri nakukaribisha. Kama uko na bwanako hiyo ni sawa, lakini si eti uzae ukiwa kwa nyumba yangu. Huyo ni mimi sasa, si Mungu,” Ng’ang’a aliongeza.