• Alisema kwamba ambo hilo limempa wasiwasi mkubwa, akidai kuwa hilo linamtokea kutokana na kwamba huko Kanada, hana mazoea ya kutumia lugha hiyo.
• Mboya alisema kwamba lugha ambazo anazungumza aghalabu ni Kiingereza, Kihispani au Kifaransa.
YouTuber Vincent Mboya amezua vichekesho kwa wakenya baada ya kudai kwamba ameanza kusahau lugha ya Kiswahili.
Mboya, ambaye anaishi nchini Kanada baada ya kuondoka nchini Kenya miezi 9 iliyopita alifunguka kupitia Instagram yake alisema kwamba maneno ya Kiswahili yameanza kumpotea kichwani.
Alisema kwamba ambo hilo limempa wasiwasi mkubwa, akidai kuwa hilo linamtokea kutokana na kwamba huko Kanada, hana mazoea ya kutumia lugha hiyo.
Mboya alisema kwamba lugha ambazo anazungumza aghalabu ni Kiingereza, Kihispani au Kifaransa.
“Ni miezi 9 sasa tangu niondoke Kenya na tayari nimeanza kusahau Kiswahili na maneno yake. Ni kama Kiswahili sasa kinaanza kupotea kutoka kichwani mwangu, siku hizi muda wote huwa nazungumza Kiingereza, Kifaransa na pengine Kispanyola. Siwezi kumbuka mara ya mwisho nilizungumza Kiswahili, nina wasiwasi,” Mboya alisema.
“Wengi wanadhani ninafanya mzaha lakini kusema ukweli niko serious,” aliongeza.
Hakuishia hapo, Mboya alienda mbele ya kupakia klipu ya video akizungumza Kiingereza na kujaribu kujieleza.
Mboya aliondoka nchini mwishoni mwa mwaka jana kuelekea Kanada katika kile wengi walidhani ni ziara ya siku chache lakini ikaja kubainika kwamba hakuwa mtu wa kurudi muda wowote hivi karibuni.