• “Jamani tusaidieni kwenye maombi…hali yake sio nzuri ila tunamuombea uponyaji,” Mr Seed aliongeza.
Msanii wa injili Mr Seed ameomba msaada wa maombi kutoka kwa mashabiki wake akielezea kwa hisia za uchungu jinsi mamake amekuwa akitaabika kutafuta matibabu.
Mr Seed alipakia video mamake akiwa amelazwa hospitalini na kueleza kwamba amekuwa akihangaika kutafuta matibabu tangu mwaka jana.
“Nimekuwa nikiingia na kutoka katika hospitali mbalimbali kwa muda wa mwaka 1 na nusu nikijaribu kutafutia mama yangu matibabu. Inasikitisha sana kuona mama yetu anateseka kila siku 💔💔 .. lakini bado Mungu ni mwaminifu na tunamtumaini na kumuombea apone,” Mr Seed alisema.
Akiwa amenyongonyea, Mr Seed alitoa wito kwa kila mtu ambaye ameona video hiyo kumkumbuka mama yake katika dua ilia pate nauu ya haraka.
“Jamani tusaidieni kwenye maombi…hali yake sio nzuri ila tunamuombea uponyaji,” Mr Seed aliongeza.
Mashabiki wake na watu mbalimbali walimpa pole na kuahidi kusimama naye wakati huu anahangaikia matibabu ya mzazi wake.
“Ugonjwa unaweza kudhoofisha familia. Kuomba kwa ajili ya mama, wewe Mr Seed na familia nzima. Umejaribu kujitia Nguvu lakini ni wazi inakulemea. Pole bro tuko pamoja,” @aileensharu.
“Mungu yuko usukani,” mpenziwe Nimo alimpa moyo.