• Hivi majuzi, kijana huyo alipokea mavazio ya viatu kwa mara ya kwanza kabisa katika maisha yake, shukrani kwa mwanasiasa Alinur Mohamed.
• Pia, aliahidiwa ziara ya kujivinjari katika jiji la Mombasa na afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya usafirisha wa watalii, Bonfire Adventures, Simon Kabu.
Msanii Justina Syokau amedai kuwa penzi lake limedondokea kwa kijana anayedaiwa kuwa mrefu zaidi nchini, Bradley Mtall maarufu kama Gen Z Goliath.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Justina Syokau alichapisha picha ya kijana huyo na kusema kwamba ndiye tafsiri kamili ya mwanamume mtanashati.
Syokau alisema kwamba Bradley na urefu wake ndiye mwanamume wa ndoto zake na kutaka afikishiwe ujumbe kwamba penzi linamtesa na anafaa amtafute wakwende wote Dubai.
“Wakati ninasema mrefu na mtanashati, huyu ndiye ninamaanisha. Huyu kijana Bradley Mtall ndiye mwanamume wa ndoto zangu na namhitaji. Mwambieni mamtafuta sababu huwa namuota,” Syokau alisema.
“Nataka niende Dubai na wewe sababu nimeishi kukupenda Bradley Mtall, Simon Kabu ratibu haya maneno,” aliongeza.
Hivi majuzi, kijana huyo alipokea mavazio ya viatu kwa mara ya kwanza kabisa katika maisha yake, shukrani kwa mwanasiasa Alinur Mohamed.
Pia, aliahidiwa ziara ya kujivinjari katika jiji la Mombasa na afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya usafirisha wa watalii, Bonfire Adventures, Simon Kabu.
Amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii katika siku za hivi karibuni kutokana na kimo kisochokuwa cha kawaida, akidai kuwa ana urefu wa zaidi ya futi 8.