“Nilitumia 10k” Mrembo aliyechora tattoo ya uso wa MP Babu Owino mwilini afunguka

“Nikikutana na yeye naweza chini kwa sababu hata kila asubuhi nikiamka jambo la kwanza namuosha uso kwa hii tattoo, nampaka mafuta namuambia ‘uko sawa?’ na kama ni chakula najua nitakula kitamfikia,” aliongeza.

Muhtasari

• Akizungumzia gharama, mrembo huyo alisema alitumia hadi shilingi elfu 10 kwa ajili ya kuchora tattoo hiyo zaidi ya saa 4.

BABU OWINO
BABU OWINO
Image: HISANI

Mrembo aliyechora tattoo ya mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amevunja kimya chake.

Akizungumza na waandishi wa habari za mitandaoni, mrembo huyo ambaye alisema anatoka katika eneo bunge la Embakasi Kusini anakubali sana sera za kisiasa za mbunge huyo kijana kutoka Embakasi Mashariki.

“Babu Owino mimi huwa nimemtambua sana kwa sababu hii sio tattoo yake nachora ya kwanza, kuna ya kwanza nilichora nikiwa kidato cha nne. Ni jamaa mwenye nimemtambua kutoka kitambo kulingana na vile vitu anafanyia watu,” alisema.

“Ukiangalia Nairobi, si watu wote wanafanya vitu vyenye Babu Owni anafanya, yeye huwa haangalii kabila, ndio maana mimi kwangu nampa bendera. Mimi siasa inakuwa kwa damu yangu sana, nikikutambua ni hivyo,” aliongeza.

Akizungumzia gharama, mrembo huyo alisema alitumia hadi shilingi elfu 10 kwa ajili ya kuchora tattoo hiyo zaidi ya saa 4.

“Tattoo ya kwanza nilichora ya Sh3,500 na hii ya pili nimechora ya Sh10,000. Nilifika saa tisa alasiri nikakaa hadi saa moja jioni nikichorwa. Hiyo pesa ni rent yangu ya miezi 2 lakini niliamua nikasema kama mbaya ni mbaya,” alisema.

Cha kushangaza, mrembo huyo alikiri kwamba licha ya kufanya hayo yote kwa ajili ya Owino, mbungev huyo hamjui hata kidogo.

“Babu Owino hanijui kabisa japo mimi namjua. Hatujawahi kutana naye lakini ningependa kukutana naye nimuone hata nimsalimie tu na mkono, hiyob tu.”

“Nikikutana na yeye naweza chini kwa sababu hata kila asubuhi nikiamka jambo la kwanza namuosha uso kwa hii tattoo, nampaka mafuta namuambia ‘uko sawa?’ na kama ni chakula najua nitakula kitamfikia,” aliongeza.