• “Sasa pumzika mpendwa wangu, nitakupenda daima,” Mr Seed aliandika.
Msanii wa injili Mr Seed amethibitisha kifo cha mama yake, ikiwa ni si9ku chache baada ya kuomba mashabiki kuwakumbuka katika maombi wakati mamake alikuwa anahangaika kutafuta matibabnu hospitalini.
Mr Seed aliwekac wazi kuhusu kifo cha mama yake kupitia Instagram ambapo aliandika ujumbe mfupi wa kumuomboleza akiahidi kumpenda hata katika kifo chake.
“Sasa pumzika mpendwa wangu, nitakupenda daima,” Mr Seed aliandika.
Hii inakuja siku nne tu baada ya msanii huyo kuchapisha ujumbe Instagram akiambatanisha na video ya mamake akihangaikiwa na madaktariv katika hospitali moja jijini Nairobi.
Mr Seed alifichua kuwa mama yake amekuwa akitafuta matibabu kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita na kuwataka mashabiki kuwakumbuka kwa dua ili mama yake apone.
“Nimekuwa nikiingia na kutoka katika hospitali mbalimbali kwa muda wa mwaka 1 na nusu nikijaribu kutafutia mama yangu matibabu. Inasikitisha sana kuona mama yetu anateseka kila siku 💔💔 .. lakini bado Mungu ni mwaminifu na tunamtumaini na kumuombea apone,” Mr Seed alisema.
Akiwa amenyongonyea, Mr Seed alitoa wito kwa kila mtu ambaye ameona video hiyo kumkumbuka mama yake katika dua ilia pate nauu ya haraka.
“Jamani tusaidieni kwenye maombi…hali yake sio nzuri ila tunamuombea uponyaji,” Mr Seed aliongeza.