“Nataka DNA!” Otesa anayedai kuwa pacha wa Bradley afunguka baada ya kutua Nairobi

Kijana huyo wa Bungoma anadai kuwa yeye ndiye mrefu kuliko Bradley akisema urefu wake ni futi 8.5 hali ya kuwa Bradley ni futi 8.3

Muhtasari

• Kijana huyo wa Bungoma anadai kuwa yeye ndiye mrefu kuliko Bradley akisema urefu wake ni futi 8.5 hali ya kuwa Bradley ni futi 8.3

MARONGO NA OTESA
MARONGO NA OTESA
Image: Hisani

Isaac Otesa Wekesa, jamaa mrefu kutoka Bungoma anayedai kuwa pacha wa Bradley Marongo kutoka Vihiga ameweka wazi kwamba anataka kukutana naye na ikiwezekana wafanyiwe vipimo vya DNA kubaini kama wao ni ndugu.

Akizungumza na YouTuber Trudy Kitui baada ya kufika Nairobi, Otesa Wekesa alisema kwamba yuko tayari kwa ajili ya DNA baada ya mama yake kumshinikiza kutoka Nyumbani Bungoma na kuja Nairobi kukutana na Bradley anayeishi mtaa wa Kangemi.

“Namtamani kama ndugu akuje tukae na yeye tuongee tujue vile tunaweza kusaidiana. Lakini mimi najua Bradley ni ndugu yangu,” alisema kwa kujiamini.

 “Nko tayari kwa ajili ya DNA,” aliongeza kwa ujasiri wa aina yake.

Akisema kwa nini aqliamua kumfuata mwenzake kuja Nairobi, Otesa alisema kwamba mama yake ndiye alimshinikiza akidai pia kuwa huenda ni kaka wa toka nitoke.

“Nilimuuliza mama, ‘mama niambie ukweli kwa sababu vitu venye iko usikuje kudanganya’. Mama akasema ‘wee toka hapa uniambie vitu hivyo, kama unaona kama kuna ndugu yako endapo utafute,” alisema.

Kijana huyo wa Bungoma anadai kuwa yeye ndiye mrefu kuliko Bradley akisema urefu wake ni futi 8.5 hali ya kuwa Bradley ni futi 8.3

Bradley alipata umaarufu kwa mara ya kwanza wakati wa maandamano ya hivi majuzi ya gen Z kote nchini, na kupata cheo cha Gen Z Goliath.