• Akitetea kauli hiyo, Natasha alisema kwamba suala la ndoa si la kuchukuliwa kwa wepesi kwani chaguo mtu analolifanya ndilo litakaloamua maisha yake ya ukubwani kama mwanandoa.
Mchungaji wa kanisa la Empowerment Christian Church, Lucy Natasha amewashauri watu ambao ni wachamungu kujitenga mbali na wale wasiomjua Mungu wakati linakuja ni suala na mahusiano na ndoa.
Akizungumza na Dr Ofweneke kwenye podkasti ya Lessons At30, Natasha alisema kwamba kaitka masuala mengine watu wako huru kujumuika na wenzao bila kujali ikiwa ni wachamungu au la, lakini inapofikia ni hatua ya kumfanya mtu mpenzi wako, sharti uzingatie suala la uchamungu.
"Unastahili kufanya nini wakati unapohusiana na watu? Unapaswa kujua kuna kiwango gani kwa sababu kuna viwango tofauti vya ukaribu na uhusiano, lakini huwezi kujitenga kwa sababu wewe ni muumini, lakini katika ndoa tu. Mimi huambia watu ikiwa wewe ni Mkristo aliyeokoka na kumcha Mungu, mwanamke au mwanamume, usioe au kuolewa na mtu asiye mjua Mungu; usifungiwe nira sawa na asiye mchamungu,” Natasha alisema kwa ukakamavu.
Akitetea kauli hiyo, Natasha alisema kwamba suala la ndoa si la kuchukuliwa kwa wepesi kwani chaguo mtu analolifanya ndilo litakaloamua maisha yake ya ukubwani kama mwanandoa.
“Linapokuja suala la ndoa, msimamo wangu uko wazi sana kwa sababu huyo ni mtu anayeamua kama mipango yako itafanikiwa au itafeli, na unahitaji mtu anayekutia moyo na kuongeza upendo wako kwa Yesu. Inapohusu uhusiano na uchumba, ni tofauti,” alisisitiza.