• Msanii huyo alisema kuwa misamiati yake, kubadilisha muonekano wa nywele na fasheni ni baadhi ya vitu vinavyompa upekee si tu Kenya bali pia kimataifa.
Stevo Simple Boy amethibitisha kwamba amejishindia fursa adimu ya kusafiri kwenda Saudi Arabia kwa ajili ya shoo kubwa shukrani kwa kauli yake ya hivi majuzi.
Akizungumza kwenye kipindi cha Hangout katika runinga ya K24 jioni ya Ijumaa, Stevo alifichua kwamba kwa sasa anajiandaa kwa ajili ya kusafiri kuenda taifa hilo la Uarabuni kutumbuiza kwa mashabiki wake.
Stevo alisema kwamba kauli ya ‘mefi mefi muskla’ ambayo alibuni hivi majuzi ndiyo imemletea mafanikio hayo, akifichua kwamba ni safari yake ya kwanza kabisa nje ya nchi katika maishayake, na hawezi kusubiri siku yenyewe kufika.
Msanii huyo alisema kuwa misamiati yake, kubadilisha muonekano wa nywele na fasheni ni baadhi ya vitu vinavyompa upekee si tu Kenya bali pia kimataifa.
“Kwa nini mimi kila mara ninabadilisha muonekano wa nywele, mavazi na pia misamiati? Unajua mimi ni msanii si Kenya peke yake, ni Afrika Mashariki nzima lakini sasa nataka kutanua mbawaq zaidi niende kimataifa,” Stevo alifafanua.
“Kwa hiyo mefi mefi muskla ni lugha ya Kiarabu, wakati nilisema hivyo, unajua nini kilifanyika? Ni bahati tu ilinitokea, mwezi ujao ninaenda Saudi Arabia kwa kusema tu ‘mefi mefi muskla’. Tarehe 23 Septemba nitakuwa napiga shoo Riyadh. Mefi mefi muskla inamaanisha hakuna shida, mambo yaki shwari,” Stevo alifafanua zaidi.