“Gharama ya rasta zangu ni elfu 10 tu!” – Stevo Simple Boy afichua

“Vile mimi nilibadilisha jinsi ya kuvaa, nilipata wafuasi wengi sana si tu hapa Kenya bali hata kutoka nje ya nchi. Usanii ni gharama lakini pia inakupasa uwe na bidii na moyo mkunjufu,” aliongeza.

Muhtasari

• Msanii huyo wa Freshi Barida alifichua kwamba ni nywele asilia aina ya rasta ambazo alizipata kwa shilingi elfu 10 tu pesa za Kenya.

STEVO SIMPLE BOY
STEVO SIMPLE BOY
Image: SCREENGRAB//K24TV

Rapa Stevo Simple Boy kwa mara ya kwanza amezungumzia kuhusu gharama ya nywele zake mpya za rasta.

Akizungumza Iju8maa alasiri kwenye runinga ya K24, Stevo Simple Boy ambaye Alhamisi alitambulisha muonekano wake wa nywele za rasta alifichua kwamba si za gharama kubwa kama ambavyo wengi walikuwa wanadhani.

Msanii huyo wa Freshi Barida alifichua kwamba ni nywele asilia aina ya rasta ambazo alizipata kwa shilingi elfu 10 tu pesa za Kenya.

“Hizi rasta ni za elfu 10 tu,” Stevo alifichua.

Akizungumzia kuhusu fasheni yake katika siku za hivi karibuni akitokea mara kwa mara na mavazi ya ajabu yanayokaa kama yanampwerepweta, Simple Boy alisema;

“Niko na designer, yeye ndiye anajua ni kitu kipi ambacho ninastahili nivae na kwa wakati upi. Iwe ninaenda kwa shjoo, interview, nikitembea mitaani. Ukiwa msanii lazima uvae tofauti na watu wengine,” Stevo alisema.

Msanii huyo alifichua kwamba kubadidisha mtindo wake wa kuvaa umempa faida nyingi zikiwemo kupata ufuasi mkubwa si tu hapa Kenya bali hata kutoka nje ya nchi.

“Vile mimi nilibadilisha jinsi ya kuvaa, nilipata wafuasi wengi sana si tu hapa Kenya bali hata kutoka nje ya nchi. Usanii ni gharama lakini pia inakupasa uwe na bidii na moyo mkunjufu,” aliongeza.