• Ronaldo ni baba kwa watoto watano na ameoana na mwanamitindo kutoka Uhispania, Georgina Rodriguez.
• Mchezaji huyo ndiye binadamu mwenye ufuasi mkubwa zaidi katika mtandao wa Instagram, na si rahisi yeye kuangalia jumbe kwenye DM zake.
Mchekeshaji chipukizi ambaye pia ni mtengenezaji wa maudui, Dem wa Facebook amemwandikia mchezaji gwiji kutoka Ureno, Cristiano Ronaldo ujumbe wenye hisia akimuomba kumpenda.
Katika ujumbe huyo ambao mrembo huyo alionyesha kupitia kurasa zake katika mitandao ya kijamii, alimbembeleza Ronaldo kumchukua kama mpango wa kando.
Dem wa FB aliingia kwenye DM ya Ronaldo ya kujimiminia sifa jinsi amekuwa shabiki wake hata kabl;a ya kuzaliwa, huku pia akitambua kuwa mchezaji huyo ana familia lakini yeye angependa kupendwa kama sidechick.
Kuhusu wasifu wake kwa mchezaji huyo wa Al Nassr ya Saudi Arabia, Dem wa FB alisema kwamba yeye pia ni mchezaji, japo si katika malimwengu ya soka bali katika kuchezea roho za wanaume wanaoonesha nia ya kumtongoza.
“Hujambo mtanasati Ronaldo, mimi ni mchekeshaji kutoka Kenya naitwa Dem wa Facebook na pia ni mwanasoka – huwa nacheza na wanaume wa Kenya. Mimi ndiye mrembo zaidi si tu Kenya bali pia Afrika kwa ujumla. Nilikuwa shabiki wako hata kabla nizaliwe, na najua uko katika ndoa yenye furaha lakini nakuomba unichukue kama mpango wa kando,” Dem wa FB alimaliza.
Ronaldo ni baba kwa watoto watano na ameoana na mwanamitindo kutoka Uhispania, Georgina Rodriguez.
Mchezaji huyo ndiye binadamu mwenye ufuasi mkubwa zaidi katika mtandao wa Instagram, na si rahisi yeye kuangalia jumbe kwenye DM zake.
Hata hivyo, Dem wa FB ana matumaini sufufu kwamba endapo itakuja kufika siku moja Ronaldo afikie na kusoma ujumbe wake, pengine atampa jibu ambalo litautuliza moyo wake.
Kila la Kheri Dem wa FB.