Mpenziwe Nicholas Kioko ajibu kwa nini hawampi yaya wao platform ya kujulikana mitandaoni

“Kuhusu suala la platform guys, unajua yaya akikuja, anakuja kufanya kazi ya nyumba. Hajakuja ndio tumpe platform. Ni sisi tu ndio tunapenda tumtag au la,” Wambo Ashley alisema.

Muhtasari

• Hivi majuzi, Kioko na Ashley walimulikwa na jicho la wanamitandao baada ya uvumi kuibuka kwamba walikuwa wanamlipa shilingi 12k kila mwezi.

WAMBO ASHLEY.
WAMBO ASHLEY.

Wambo Ashley, mpenziwe YouTuber Nicholas Kioko amevunja kimya kuhusu ni kwa nini hawapendi kumjumuisha mfanyikazi wao wa ndani katika video za familia yao kwenye YouTube.

Kupitia kipindi cha maswali na majibu na mashabiki wake, mmoja alilenga kujua ni kwa nini yaya wao hana platform katika mitandao ya kijamii kama yaya wanaofanya kazi kwenye maboma ya wanandoa wengine maarufu mtandaoni.

Kwa mujibu wa Ashley, kwani wanaamini kwamba yaya anapoajiriwa kazi, kazi yake ni kushughulika na masuala ya nyumbani na wala si kutumia kama njia moja ya kujizolea umaarufu kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuhusu suala la platform guys, unajua yaya akikuja, anakuja kufanya kazi ya nyumba. Hajakuja ndio tumpe platform. Ni sisi tu ndio tunapenda tumtag au la,” Wambo Ashley alisema.

Mama huyo wa mapacha alifichua kwamba yaya wake wa awali alikuwa ni mtu hapendi kuonekana kwenye kamera, na hivyo walichukua kutoka hapo kwamba yaya wote pengine hawapendi kuonekana kwenye kamera.

“Hata hivyo, sina shida na kumpa mtu platform lakini kulingana na uzoefu niliopata kutoka kwa yaya wangu wa awali yeye hakuwa anapenda kuonekana kwenye kamera kabisa,” Wambo alisema.

Hivi majuzi, Kioko na Ashley walimulikwa na jicho la wanamitandao baada ya uvumi kuibuka kwamba walikuwa wanamlipa shilingi 12k kila mwezi.

Hata hivyo, ni uvumi ambao wanandoa hao waliupuuza wakisema kwamba hawajui nani alianzisha tetesi hizo kwenye mitandao ya kijamii.