Nuru Okanga atikisa kijiji Kakamega baada ya kununua ‘kisiagi’ (video)

Wanakijiji wenye furaha walionekana wakiimba na kucheza densi na Okanga huku wamebeba kisiagi kabla ya kufanya maombi Mungu kubariki kazi ya Okanga kuwahudumia wanakijiji.

Muhtasari

• Okanga alinunua kinu hicho, siku chache baada ya kukabidhiwa pesa na mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ambaye alimuahidi kumsaidia.

ndani ya studio za Radio Jambo.
Nuru Okanga ndani ya studio za Radio Jambo.
Image: RADIO JAMBO

Mwanasiasa Nuru Okanga alisimamisha kijiji katika wadi ya Kholera kaunti ya Kakamega baada ya kuwasili na kinu cha kusiaga nafaka.

Okanga alinunua kinu hicho, siku chache baada ya kukabidhiwa pesa na mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ambaye alimuahidi kumsaidia.

Katika picha zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii, Okanga ambaye alikuwa juu ya gari alikaribishwa kijijini kishujaa na makumi ya watu huku akiwa na kisiagi hicho.

Mwezi uliopita, Okanga walikutana na Sudi katika kipindi cha Obinna kwenye YouTube na mbunge uyo alimtaka Okanga kusema anacotaka kufanyiwa naye ili kubadilisha maisha yake.

Okanga aliomba Sudi kumpa shilingi milioni moja kwa ajili ya kuanzisa biashara, kununua kinu cha kusiaga nafaka na kufungua duka yakiwa maazimio yake.

Klipu hiyo ilimnasa akiwa amesimama nyuma ya lori lililokuwa limebeba kinu cha kusiaga, akiangazia furaha na sherehe iliyozunguka kuwasili kwake.

“Sasa tukija kwa mimi kama Nuru Okanga, ile familia nimetoka mimi ndio kama tegemeo la kila mtu. Mwenyewe sina kazi, shida zangu nikieleza zote ni nyingi lakini nataka niende kwa moja mahsusi. Mheshimiwa kwa roho nzuri yako Mungu akuingie, kama unaweza nipatie Sh1m, biashara yangu itakuwa sawa kabisa.”

“Nitaenda niweke biashara yangu na nitulie, nyumbani kwetu mahali nimezaliwa hakuna kisiagi, nitanunua kisiagi niweke hapo. Hapo kwetu hakuna duka karibu, hivyo nitaweka duka na pia nitaweka biashara ya mambo ya kutengeneza fenicha na eneo la kuoshea magari na pikipiki,” aliongeza.