Tukipendana na Arrow Bwoy bado nilikuwa na mpenzi mwingine – Nadia Mukami

“Mpenzi wa awali hakuwa amenioa, na hatukuwa na watoto pamoja, tulikuwa tu wapenzi. Alikuja kugundua mitandaoni kwamba tuna’date na Arrow Bwoy, akanitext nikamblock na ikaisha hivo,” Nadia alisema.

Muhtasari

• Akiulizwa kwa nini aqliamua kufanya hivo bila kujali hisia za mpenzi huyo mwingine, Nadia Mukami alisema kwamba huyo akuwa amemuoa rasmi na pia hawakuwa wamepata watoto.

Nadia Mukami na Arrow Bwoy
Image: HISANI

Malkia wa miziki ya kizazi kipya humu nchini, Nadia Mukami amefichua kwamba aliingia katika uhusiano wa kimapenzi na Arrow Bwoy kama bado angali kwenye uhusiano mwingine.

Akizungumza na mkuza maudhui Oga Obinna, Nadia Mukami alisema kwamba mapenzi yao yalianza wakati kila mmoja kati yake na Arrow Bwoy alikuwa bado kwenye mahusiano mengine ya kimapenzi.

Akiulizwa kwa nini aliamua kufanya hivo bila kujali hisia za mpenzi huyo mwingine, Nadia Mukami alisema kwamba huyo akuwa amemuoa rasmi na pia hawakuwa wamepata watoto.

“Wakati nilianza kuchumbiana na Arrow Bwoy, nilikuwa ninatoka kazi, huo wakati tulikuwa tumeanza kuwa na issues na mpenzi wa zamani. Nilikuwa natafuta mtu wa kunisaidia kusukuma kazi zangu za muziki. Arrow alinitext akiniuliza niko wapi. Hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza tulianza kuchumbiana,” alisema.

“Tulikuwa tunazungumza hapo awali, na kipindi hicho chote yeye alikuwa kwenye uhusiano kabisa na mimi nilikuwa katika uhusiano wangu pia. Aliniuliza kama niko tayari kuchumbiana naye, nikamwambia hakuna shida, na hivyo ndivyo tulianza kupendana.”

“Mpenzi wa awali hakuwa amenioa, na hatukuwa na watoto pamoja, tulikuwa tu wapenzi. Alikuja kugundua mitandaoni kwamba tuna’date na Arrow Bwoy, akanitext nikamblock na ikaisha hivo,” Nadia alioongeza.

Hata hivyo, mama huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba ilimkalia rahisi kuachana na uhusiano huo wa zamani na kukumbatia uhusiano mpya na Arrow Bwoy kwa sababu walikuwa wameanza kuwa mbali kutoka kwa kila mmoja.