“Bado mimi ndiye content GOAT” – Nicholas Kioko ajibu tetesi za kuacha content creation

“Nimepost video leo, ni vile mimi bado ndiye content GOAT, mimi bado ndiye Senior Udaku Reporter. Ni kweli sijakuwa nikipandisha video sana kama kitambo lakini wenye wamekuwa sijaona kitu wamekuwa wakifanya."

Muhtasari

• Akizungumza na SPM Buzz, Kioko alikanusha uvumi huo na kusema kwamba bado yeye ndiye yule yule kinara katika kufanya maudhui ya burudani humu nchini.

NICHOLAS KIOKO.
NICHOLAS KIOKO.
Image: FACEBOOK.

YouTuber Nicholas Kioko amevunja kimya chake kuhusu tetesi za mitandaoni kwamba ameacha ukuzaji maudhui.

Akizungumza na SPM Buzz, Kioko alikanusha uvumi huo na kusema kwamba bado yeye ndiye yule yule kinara katika kufanya maudhui ya burudani humu nchini.

Hata hivyo, Kioko alikiri kwamba katika siku za hivi karibuni amepunguza kasi ya kufanya content creation kupitia YouTube lakini akajitangaza kama mmoja wa YouTubers wakuu nchini bado.

“Nimepost video leo, ni vile mimi bado ndiye content GOAT, mimi bado ndiye Senior Udaku Reporter. Ni kweli sijakuwa nikipandisha video sana kama kitambo lakini wenye wamekuwa sijaona kitu wamekuwa wakifanya. Kama siko hakuna udaku,” Kioko alisema.

Baba huyo wa mapacha alisema kwamba hana mpango wa kuacha kufanya content creation kwa sasa, akifichua kwamba pengine atafikiria kuachia kipaza sauti atakapofikisha umri wa miaka 40 kuendelea.

Kuhusu afya ya mwili wake, Kioko alifichua kwamba amekuwa akipambana na ugonjwa na hivi majuzi ameafikia uamuzi wa kuacha hata kutumia pombe kabisa akilenga pia kukata uzani wa mwili wake.

“Nilikuwa nafanya physiotherapy sessions nilimaliza, lakini bado sijaheal kabisa lakini naendelea kupambana. Wakati mwingine niko sawa wakati mwingine siko sawa. Kuna vitu vingi nimeacha kufanya kwa mfano siwezi beba kitu kizito, nimebadilisha jinsi ya kulala, siwezi keti chini kwa muda mrefu, pia nimeacha kutumia pombe juu nataka kupunguza weight pia,” alisema.