Marya Okoth athibitisha kuvunjika kwa ndoa yake na mchekeshaji YY

Katika mahojiano ya awali, Mkewe YY, Marya Okoth, alisema walianza kuishi pamoja saa moja baada ya kukutana kwa mara ya kwanza.

Muhtasari

• Katika mahojiano ya awali, Mkewe YY, Marya Okoth, alisema walianza kuishi pamoja saa moja baada ya kukutana kwa mara ya kwanza.

YY NA MPENZIWE MARYA
YY NA MPENZIWE MARYA

Marya Okoth, mpenzi wa mchekeshaji YY amewavunja nyoyo mashabiki wa ndoa yao baada ya kutangaza kwamba wamefikia uamuazi wa kuachana.

Kupitia Instagram, Marya alichapisha ujumbe mfupi akiwataarifu mashabiki wake kwamba kuanzia sasa kwenda mbele, hatokuwa tena anahusishwa kwa njia yoyote na YY.

Alisema kwamba uamuzi wa kuachana ni kutokana na sababu zisizoweza kuepukika huku akijuta kwa kuwavunja mioyo mashabiki ambao walikuwa wanashabikia uhusiano wao.

“Hamjambo na habari za asubuhi, tunasikitika kuwataarifu kwamba Marya Okoth na YY hawatokuwa pamoja tena kutokana na sababu zisizoweza kuepukika. Shukrani kwa upendo na uungwaji mkono wetu katika safari ya uhusiano wetu. Tunatumai kila mmoja wetu ataheshimu faragha yetu, ahsante,” Marya alisema kwenye waraka huo.

Katika mahojiano ya awali, Mkewe YY, Marya Okoth, alisema walianza kuishi pamoja saa moja baada ya kukutana kwa mara ya kwanza.

Akiongea na Mic Check Podcast, Marya alisema alihamia nyumbani kwa YY mara tu baada ya date yao ya kwanza. Wamekuwa pamoja tangu wakati huo na wana binti wa miaka mitatu, Circe Gaona.

Marya alielezea kwa utani kwamba mcheshi huyo mashuhuri alimshinda wakati wa tarehe, lakini wote wawili walijitolea kutumia maisha yao pamoja.