“Kwetu kuwa na boyfriend sio big deal, ni kujaribu tu mambo mapya!” – binti wa Kanyari

Katika kile kilichoonekana kuwashangaza wengi, binti huyo anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 12 alidai kwamba katika familia yao, suala la kuwa na boyfriend ni la kawaida tu kwani ni kama kujaribu mambo mapya.

Muhtasari

• “Binti yangu, unaweza kudanganya kuhusu kitu chochote lakini usijaribu kudanganya kuhusu kuwa na boyfriend. Katika umri wako suala la kuwa na boyfriend katika nyumba yangu ni Hapana,” alisema.

• Hata hivyo, Sky alisisitiza kwamba hajasema uongo wowote, akisema kwamba babake wa kufikia ndiye aliyemshauri kuwa na boyfriend.

SKY VICTOR KANYARI
SKY VICTOR KANYARI
Image: INSTAGRAM

Sky Victor, binti wa kwanza wa mchungaji mtatanishi Victor Kanyari na aliyekuwa mke wake, msanii Betty Bayo ameshangaza mashabiki wake baada ya kudai kwamba katika familia yao, baadhi ya masharti makali kwa watoto yamelegezwa.

Katika video moja ambayo imeenzwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo alikuwa anarekodi akiwa kwenye gari na wazazi wake, Betty Bayo na baba wa kambo Hiram Gitau na kakake mdogo, aliwasifia wazazi hao akisema kwamba kwake wamemrahisishia maisha.

Katika kile kilichoonekana kuwashangaza wengi, binti huyo anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 12 alidai kwamba katika familia yao, suala la kuwa na boyfriend ni la kawaida tu kwani ni kama kujaribu mambo mapya.

‘Katika familia yetu, kuwa na boyfriend hata si suala nyeti vile, ni kama tu kujaribu mambo mapya. Kwetu sisi ni jambo la kawaida tu,” Sky alisema huku wazazi wake waliokuwa wameketi kiti cha nyuma kwenye gari wakiangaliana kwa mshangao.

Baada ya kuundua kwamba kila mmoja alipigwa na mshangao na kuamua kusalia kimya, Sky aliwauliza mbona hawasemi chochote akiwaambia wanamuabisha kwa kukaa kimya.

Hapo ndipo mamake, alimkata kalima na kumwambia kwamba yuko huru kudanganya kuhusu kila kitu lakini si kuhusu uhuru wa kuwa na boyfriend katika nyumba yake.

“Binti yangu, unaweza kudanganya kuhusu kitu chochote lakini usijaribu kudanganya kuhusu kuwa na boyfriend. Katika umri wako suala la kuwa na boyfriend katika nyumba yangu ni Hapana,” alisema.

Hata hivyo, Sky alisisitiza kwamba hajasema uongo wowote, akisema kwamba babake wa kufikia ndiye aliyemshauri kuwa na boyfriend.