Alikiba afichua kwa nini hana mazoea ya kuwekwa mambo yake hadharani mitandaoni

“Ni kwa sababu hivyo ndivyo nilivyo na hivyo ndivyo nilivyoji’brand kutoka zamani. Hata thamani ya nyumba yangu, gari langu na hata mavazi yangu watu hawajui,” Alikiba alisema.

Muhtasari

• “Ni kwa sababu hivyo ndivyo nilivyo na hivyo ndivyo nilivyoji’brand kutoka zamani. Hata thamani ya nyumba yangu, gari langu na hata mavazi yangu watu hawajui,” Alikiba alisema.

ALIKIBA.
ALIKIBA.
Image: HISANI

Msanii wa muda mrefu wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba, maarufu kama Alikiba amefichua sababu ya kuweka maisha yake ya kibinafsi mbali na maisha ya muziki na umaarufu.

Akizungumza na waandishi wa habari za burudani kuelekea uzinduzi wa programu za kituo chake cha runinga – Crown TV, msanii huyo alisema kwamba yeye ni tofauti sana na wenzake kina Diamond, Harmonzie, Rayvanny na wengine kiasi kwamba hakuna mtu anayejua familia yake wala gharama ya nyumba yake.

Akitetea hulka hiyo yake ya kipekee, Alikiba alisema kwamba ndio mtindo wake na amezoea hivyo tangu alipopata umaarufu miaka zaidi ya 18 iliyopita.

“Ni kwa sababu hivyo ndivyo nilivyo na hivyo ndivyo nilivyoji’brand kutoka zamani. Hata thamani ya nyumba yangu, gari langu na hata mavazi yangu watu hawajui,” Alikiba alisema.

Mkurugenzi huyo wa Kings Music alionekana kuwafuma kwa mkuki baadhi ya watu wanachapisha mitandaoni kuhusu kujua utajiri na vitu wanavyomiliki watu maarufu, akisema kwamba yao huwa ni kukadiria tu lakini wengi watumia kuwahadaa watu.

Hata hivyo, alisema kuwa huwa hapendi kuwafuatilia watu hao na kuwakosoa kwani anaelewa ni waandishi wa habari za burudani ambao wanatafuta unga kupitia habari hizo hata kama ni za uongo kwa kiasi kikubwa kuhusu mali ya mastaa wanaowafuatilia.

“Wengi wenu hukadiria tu. Kuna watu mnaweka vitu feki kwenye mitandao kuhusu utajiri wa vitu vya watu lakini hmjui vitu vingi sana. Lakini pia naelewa kwamba ni content kwa sababu ndio kazi yenu,” alisema.

Alikiba ni mmoja wa wasanii ambao wameweka mpaka unoonekana kabisa baina ya maisha yake ya kibinafsi ya yale ya ustaa, kwa miaka mingi ambayo amekuwa kwenye gemu, akitajwa kama msanii ambaye ni nadra kumpata akitumia kiki kuendesha mambo yake.