Kwetu kuenda shule ni chaguo la mtu, sio lazima! – binti wa Kanyari na Betty Bayo

Binti huyo wa miaka 12 alifichua kwamba wazazi wake – Hiram Gitau na Betty Bayo – ndio wazazi wazuri kwani huwa hawamlazimishi kuenda shule, na kusema suala la shule ni chaguo la mtu tu.

Muhtasari

• Mtoto huyo alionyesha kushangazwa kwake na wazazi ambao wanawasukuma wanao kuwa suala na kuhudhuria masomo shuleni ni jambo la lazima.

• “Mimi hushangazwa na wazazi ambao wanawalazimisha wanao kuenda shule. Shule sio lazima, nyumbani mimi nahisi shule sio lazima kwangu,” alisema.

SKY VICTOR KANYARI
SKY VICTOR KANYARI
Image: INSTAGRAM

Bintiye msanii wa Kigooco, Betty Bayo na mchungaji Victor Kanyari, Sky ameelezea jinsi anafurahia uhuru wa kulelewa na babake wa kambo, Hiram Gitau.

Akizungumza kupitia chaneli yake ya YouTube, Sky alikuwa anahadithia jinsi familia yake inampa uhuru maradufu katika kufanya baadhi ya vitu, tofauti na familia zingine.

Binti huyo wa miaka 12 alifichua kwamba wazazi wake – Hiram Gitau na Betty Bayo – ndio wazazi wazuri kwani huwa hawamlazimishi kuenda shule, na kusema suala la shule ni chaguo la mtu tu.

“Najua si watoto wote wanapata upendeleo kama huu lakini mimi nina uhuru wa kufanya chochote kwetu. Unajua maisha ni kwa ajili ya wanaoishi. Siwezi kuwaelezea wazazi wangu kama wale wa Kiafrika kabisa, hapana, mimi nina uhuru wa kula, kulala na kufanya chochote wakati wenye nataka mwenyewe,” Binti huyo alianza kueleza.

“Hata kama ni siku ya shule nina uhuru wa kulala tu ninavyotaka na ninahisi kwamba uhuru kama huo ni wa kipekee. Nahisi pia kwamba wazazi wangu ni watu wa kuelewa sana, kwa sababu kama sijihisi kuenda shule wananikubalia wanasema ni sawa. Kama sitaki kuenda shule ni chaguo tu na nafikiri hiyo ndio njia sahihi kwa watoto siku hizi kwa sababu mtu unaweza amka unajihisi hutaki kuenda shule, na mimi wazazi wangu huwa hawana tatizo na hilo,” aliongeza.

Mtoto huyo alionyesha kushangazwa kwake na wazazi ambao wanawasukuma wanao kuwa suala na kuhudhuria masomo shuleni ni jambo la lazima.

“Mimi hushangazwa na wazazi ambao wanawalazimisha wanao kuenda shule. Shule sio lazima, nyumbani mimi nahisi shule sio lazima kwangu,” alisema.

Katika mfululizo huo wa maisha yake na wazazi wake, awali tuliripoti kwamba Sky aliwashangaza hata wzazi wake alipofichua kwamba ana uhuru wa kuwa na mpenzi katika umri huo wake mdogo.