Bradley Mtall ajawa bashasha baada ya kuvaa viatu kwa mara ya kwanza maishani mwake

Bradley ameshukuru kuvishwa viatu kwa mara ya kwanza maishani mwake

Muhtasari

•Bradley Mtall anashukuru Bata kwa kumvisha viatu vilivyofungwa kwa mara ya kwanza maishani mwake

•Mwezi uliopita Bradley alitembelea makao makuu ya Bata ili apimwe vipimo vya viatu

Bradley Mtall
Bradley Mtall
Image: thegenzgoliath//Instagram

Bradley Mtall anashukuru kampuni ya Bata kwa kumvisha viatu vya kamba kwa mara ya kwanza maishani mwake.

Mwezi uliopita Bradley alitembelea makao makuu (HQ) ya Bata ili apimwe vipimo vya viatu baada ya kusema kwa kuwa ameishi kuvaa 'akalaa' na hizo ndizo viatu zake za kila siku kwani hakuna kiatu kinachomtosha.

“Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya kutengeneza viatu ya Bata kwa fursa hii ya kubadilisha maisha yangu kabisa,fursa ya kuvaa viatu vilivyofungwa kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Hii ina maana kubwa zaidi kwamba ambayo hata ninakosa maneno ya kuelezea, na kwa kweli ninashukuru sana jitihada zenu. Ninatazamia kufanya kazi zaidi na nyinyi kwenye miradi mingi na yenye maana siku zijazo,” Bradley aliandika.

Mwakilishi wa duka la Bata aliulizwa kama Bradley ndiye wa kwanza kushonewa viatu kubwa ambapo alijibu kwamba sio wa kwanza kwani kuna watu wenye miguu mikubwa.

Aliendelea na kueleza kuwa wakati viatu vya kupimwa hutengenezwa, wao hujaribu kufanya ziweze kudumu kwa muda mrefu kwa sababu wanajua ni ngumu kwa watu wenye miguu mikubwa kupata viatu.