Commentator na mkewe waweka sura ya mwanao mtandaoni

Wanandoa hao walibarikiwa na mtoto tarehe 13 Machi

Muhtasari

• Familia ya Commentator inajiunga na familia nyingine za mastaa nchini kufanya sherehe za utamblisho wa sura za wanao kwa umma.

Image: IG// commentator_254

Mtengenezaji wa maudhui ya mtandaoni Commentator 254 pamoja na mke wake wameweka wazi sura ya mtoto wao santiago.

Wawili hao wamechapisha picha katika ukurasa wao wa Instgram dakika chache baada ya sherehe ya kumtambulisha mwanao kwa jamii ya mtandaoni.

Alhamisi, Commentator alitangaza kuwa kungekuwa na sherehe ya kumtambulisha Santiago maarufu kama face reveal.

"Utambulisho huu wa sura huwezi kosa. Hii ndio bora zaidi nchi hii imewai kuwa nayo juu imehaririwa wa wako mkweli Mzee Comme." Aliandika Commentator 254.

Wanandoa hao walibarikiwa na mtoto tarehe 13 Machi na tangu wakati huo, wamekuwa wakificha sura ya mtoto kwenye picha walizokuwa wakibandika mtandaoni.

Mtoto huyo licha ya umri mdogo alifunguliwa kaunti ya Instagram ambayo tayari ina wafuasi.

Mkewe Commentator 254, Moureen Ngigi kwa upande wake ameelezea furaha yake kwa maneno machache akisema, "mtoto wetu urithi wetu."

Familia ya Commentator inajiunga na familia nyingine za mastaa nchini kufanya sherehe za utamblisho wa sura za wanao kwa umma.

Hivi maajuzi, familia ya The Bahati's ilimtambulisha mwanao kwa umma sawia na wanandoa Carey Priscilla na Benito Muriu.