Msanii Barobaro asimulia jinsi aliwachwa baada ya kulipa mahari

Alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na binti mmoja ambaye mamake alikuwa rafiki wake wa dhati

Muhtasari

• Barobaro alilipa mahari ya shilingi laki tano kwa familia ya binti aliyempachika ujauzito.

• Awali hakujua kuwa binti aliyekuwa anamchumbia alikuwa mtoto wa rafiki wake wa karibu sana.

Msanii Barobaro
Image: IG//barobaro_tz

Msanii wa muziki kutoka Tanzania Barobaro ameelezea jinsi katika maisha yake amepata changamoto wakati akiwa katika mahusiano ya kimapenzi licha ya watu kutojua.

Barobaro alieleleza kuwa amebarikiwa na nyota ya mapenzi kwa wanawake kwani kuilingana naye ni kuwa akipendwa anapendeka kiasi cha kuchanganyikiwa.

Ijapokuwa hakutarajia kupitia kipindi kigumu katika mahusiano hatimaye yalimkuta.

Msanii huyo amesema kuwa wakati wa kuanza urafiki na mama wa binti mmoja hakujua kuwa alikuwa na binti ambaye baadaye alikuwa mpenzi wake.

Baadaye alikutana na binti pamoja na mamake akamtambulisha.

Mtunzi huyo wa kibao cha Mchumba Msebule alikiri kuwa alianza mahusiano na binti yule kisha baadaye akamjulisha mamake ambaye alikuwa rafiki wake wa dhati. Hapo ndipo aliambiwa kuandka barua rasmi ya kuomba ndoa na binti yule.

Katika barua aliyoandika kwa mamake binti, Barobaro alikiri kulipa mahari ya shilingi milioni moja ila hakuwa na hela wakati ule jambo liliyombidi kuandaa tumbuizo la mziki kupata hela ya mahari.

 Wakati huo wote, Barobaro alikuwa ni mhudumu wa bodaboda na msanii na tayari alikuwa kashampachika binti ya rafiki wake ujauzito.

Hata  hivyo baada ya kulipa awamu ya kwanza ya mahari takribani shilingi laki tano, Barobaro alisema kuwa mpenzi wake alimzingua ila hakuelezea changamoto hasa ya aliyofanyiwa.