Msanii wa muziki wa kizazi kipya Otile Brown amewaonya mashabiki wake kuwa makini dhidi ya matapeli wanaotumia jina lake kuwaibia watu kwenye mtandao wa facebook.
Onyo la Otile Brown linajiri baada ya mtu mmoja kulaghaiwa shilingi laki tatu, kutoka kwa mtu aliyejifanya kuwa msanii huyo kwenye mtandao wa meta.
Kwa mujibu wa Otile Brown, ameshangazwa ni kwa nini mtu aliyelaghaiwa hakumfikia kwa wakati kuhakikisha dili iliyokuwa inapigwa licha ya kufahamu kurasa zake rasmi za Instgram na Tik Tok. OB ameshangazwa na na jinsi jamaa aliyelaghaiwa kumlaumu vikali na kuamini kuwa ni yeye(OB) aliyemlaghai.
“Si haki sasa unajua jinsi ya kunipata baada ya kulaghaiwa wakati ungenipata kwenye kurasa zangu rasmi kabla ya kulaghaiwa kimapenzi.” Alisema Otile Brown.
Msanii huyo amemtaka mtu aliyelaghaiwa kuwasilisha ushahidi kwa maafisa wa ujasusi wa DCI ili wamsaidie kupata haki. Otile Brown alisema kuwa yeye ni mtu mwenye shughuli nyingi na sio jukumu lake kuripoti kisa hicho kwenye idara ya ujasusi ya DCI.
“Nenda wasilisha ushahidi wako kwa DCI wakusaidie kupata aliyekulaghai. Sitakufanyia kazi hiyo, niko na mambo mengi ya kufanya.” Alisema Otile Brown.
Hata hivyo, Otile alimhurumia mtu aliyelaghaiwa huku akimtaka kufanya uchunguzi wa kina kabla ya kulaghaiwa.
Otile Brown aliweka wazi kuwa hana akaunti kwenye mtandao wa
facebook ila yeye hutagusana na mashan=biki wake kupitia mitandao ya Tik Tok na
Instagram.