logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kijana kwenye video ya "ameuza airport" asimulia alivyopoteza meno ya mbele

Henry Omondi amefunguka kuhusu maisha yake katika mahojiano ya kipekee na Radio Jambo.

image
na Samuel Mainajournalist

Mastaa wako29 November 2024 - 15:36

Muhtasari


  • Henry alisimulia jinsi meno yake yalivyovunjika akieleza kwamba alianguka chini baada ya kuruka na mdomo wake kugonga chini.
  • Akizungumzia maisha yake, alifichua kuwa anatoka eneo la Nyanza.


Henry Omondi, kijana katika video iliyovuma mtandaoni ya ‘ameuza airport, ameuzia Mhindi’, amefunguka kuhusu maisha yake katika mahojiano ya kipekee na Radio Jambo.

Katika mahojiano hayo, kijana huyo ambaye alisema ana umri wa miaka 19, alijibu swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza tangu aanze ku-trend wakati wa maandamano ya nchi nzima; Jinsi gani alipoteza meno yake ya mbele?

Henry alisimulia jinsi meno yake yalivyovunjika akieleza kwamba alianguka chini baada ya kuruka na mdomo wake kugonga chini.

“Nilikaa Kisumu kabla nikuje Nairobi. Siku moja mtu aliniokota na kunipeleka katika kituo cha polisi cha Nyalenda. Vile nilifika huko, hao askari wakaninunulia chakula, maji, na wakaninunulia kila kitu. Alafu wakaniweka nyuma peke yangu. Nilikaa huko ndani walitaka kunipeleka rumande, nikahisi sitaki kurudi huko juu nimewahi kuwa huko tena. Nilihisi kuruka. Nilitarajia kuruka kwa matuta, sikuruka. Vile nilitaka kuruka nilitupa maji yangu na nini, kufika mbele kitu ikinifunika macho nikashtukia nisharuka.  Nikaruka kwa uvimbe, nikaruka na mdomo wangu,” Henry alisimulia.

Kijana huyo alisema mpita njia alimchukua na kumpeleka nyumbani kwake kwa ajili ya huduma ya kwanza kabla ya kumpa chakula ambacho alikataa.

Alisema kisha alipelekwa kwenye nyumba ya watoto ambako alikaa kwa muda.

Henry alijipatia umaarufu wakati wa maandamano ya Gen-z katikati ya mwaka huu kwa kupinga vikali uuzaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Sauti yake kubwa na shauku yake wakati wa majaribio ya kuandamana hadi JKIA katika lengo la kupinga kuuzwa kwake vilimfanya kuonekana sana na video yake imekuwa ikivuma kwenye mitandao ya kijamii tangu wakati huo.

Akizungumzia maisha yake, alifichua kuwa anatoka eneo la Nyanza.

Kijana mmoja alijipatia umaarufu mkubwa wakati wa maandamano ya Gen-z katikati ya mwaka kwa kupinga kwa sauti kubwa kuuzwa kwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

“Kwa majina naitwa Henry Omondi kutoka Siaya. Nilizaliwa 2005, niko na miaka kumi na tisa sasa hivi,” alisema.

Henry alifichua kuwa yeye ni mzaliwa wa kwanza katika familia ya ndugu watano.

Alisema kuwa kwa sasa anasomea kozi ya ufundi wa umeme katika shule ya Ndere Polytechnic iliyoko North Gem, kaunti ya Siaya.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved